Habari na Angelica Sullusi,Mbeya.
Baadhi ya wananchi mkoani Mbeya wametaka bajeti ya Serikali inayotarajiwa kusomwa Bungeni wiki ijayo isaidie kupunguza mfumuko wa bei nchini ili kuwapunguzia wananchi makali ya maisha.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hii kwa nyakati tofauti Jijini Mbeya, wanachi hao wamesema kuwa mfumko wa bei ndio chanzo kikubwa cha watanzania kuwa na maisha magumu, hivyo Serikali inapaswa kulipatia tatizo hilo kipaumbele katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha.
Waziri Elimu wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji,Bwana Milanzi Petro amesema ili bajeti ijayo iwanufaishe wananchi, ni lazima wizara zinazoigusa jamii moja kwa moja zipewe kipaumbele ili ziwe na uwezo wa kuwahudumia wananchi.
Amesema ili kupunguza tatizo la mfumko wa bei Serikali itoe kipaumbele cha bajeti kwenye wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ili iwe na uwezo wa kuwahudumia wananchi katika kuinua kilimo na hatimaye kuongeza uzalishaji wa mazao na kupunguza bei za mazao.
Nae, Mwanafunzi wa mwaka wa mwisho katika Chuo Kikuu Huria (OUT) Tawi la Mbeya,Bwana Eddo Mwamalala amesema kuwa bejeti ijayo inapaswa kuja na vitu vitakavyosaidia kupunguza na kudhibiti mfumuko wa bei.
Wiki ijayo vikao vya Bunge la 10 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania vinaanza mjini Dodoma kwa ajili ya kupokea, kujadili na kupitisha makadirio ya bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2012/13.
No comments:
Post a Comment