Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, June 14, 2012

AKAMATWA NA GOBOLE KINYUME CHA SHERIA


Habari na Ezekiel Kamanga,Chunya.
Mkazi mmoja wa Kijiji cha Mbangala,Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya,Bwana Issah Malala(32) anashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kukutwa na silaha aina ya gobole nyumbani kwake.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo Diwani Athuman,amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa majira ya saa 3:00 usiku,Juni 11 mwaka huu na kwamba alikuwa anamiliki silaha hiyo kinyume cha sheria.

Ameongeza kuwa mtuhumiwa bado anashikiliwa na jeshi lake na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani ili kujibu shtaka la kumiliki silaha hiyo bila kibali.
 Pichani ni gari lenye nambari T 491 ATR lililoharibiwa na madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda,likiwa limeharibiwa vibaya kwa kuvunjwa vioo vyote Juni 9 mwaka huu,majira ya saa nne asubuhi baada ya kumgonga dereva mwenzao Mtaa wa Kabwe,Jijini Mbeya hapa kisha kutokomea.
 Lakini madereva bodaboda hao walimfukuzia mpaka Mtaa wa Mama John,Jijini humo,ambapo walimpiga baada ya kukataa kutii amri ya kulipeleka gari polisi.Hata hivyo hivi sasa Jeshi la Polisi wanawatafuta vijana wa bodaboda wanaotuhumiwa kuharibu gari hilo.

No comments: