Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, June 14, 2012

WANAFUNZI WA SHULE YA SEMINARY MANOW RUNGWE WASABABISHA HASARA YA MILIONI 50 BAADA YA KUKOSA WALI

Wanafunzi wa shule ya sekondari Manow wakiwa chini ya ulinzi wa polisi shuleni hapo

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Chrispin Meela akiwatuliza jazba wanafuzi wa manowHaya si makaratasi au takataka bali ni mitihani iliyochanwachanwa na wanafuzi haoWanafunzi wa shule ya Seminary Manow Wilayani Rungwe mkoani Mbeya usiku wa kuamkia leo wamefanya uharibifu wa kuvunja mali ya shule pamoja na kuiba vitu visivyo pungua dhamani ya shiringi milion 50.Akiongea na mwandishi mkuu wa shule hiyo ya Manow  Watson Masiba amesema kuwa mgomo huo ulianza mchana kwa kuwa wanafunzi hawakutaka kula Ugari bada ya uongozi kuwaarifu kuwa siku hiyo hakutakuwa na ratiba ya wali kwa kuwa mchele siku hiyo ulikuwa kidogo stoo,uongozi wa shule ulipojitahidi kusuruhisha suala hilo kwa kaandaa chakula hicho usiku huo lakini wanafunzi hao walianza kufanya vulugu kwa kuvunja vioo vya majengo na kuvunja milango na kuiba computa 11 za shule pamoja na kuingia katika chumba cha kuandalia mitihani na kuchana mitihani yote iliyo andaliwa kwa ajili ya kuanza kuifanya hapo kesho tarehe 15.06.2012. 

kwa mujibu wa maelezo ya wanafunzi na wana kijiji wanao izunguka shule hiyo imejionyesha kuwepo kwa tofauti kati ya uongozi wa shule na wanafunzi hivyo kufikia wanafunzi hao kutafuta sababu ya kufanya vulugu kwa kiasi cha uharibifu wa mari za shule na kanisa.akiongea na mwandishi Askofu Dr Esrael Mwakyolile amesema kuwa uharibifu ni mkubwa sana na zaidi ya mali zisizo pungua shiringi milion 50 zimeharibiwa hivyo ameitaka serikali kupitia vyombo vya dola kuchukua hatua kwa wale watakao bainika kuhusika na tukio hili kulipa fidia pamoja na kuwa uongozi wa shule utawachukulia hatua za kinidham.Naye mkuu wa wilaya ya Rungwe Chrispin Meela kwa kushirikiana na kamati yake ya ulinzi na usarama amekemea vikali kitendo kilicho fanywa na wanafunzi hao  ukizingatia shule hiyo ni ya kanisa la kiinjili la Kilutheri hivyo kuwa mfano wa tabia njema kuliko kuchukua hatua za Kigaidi kuharibu majengo na kuiba mali za shule. Bwana Meela amechumkua hatua ya kuifunga shule hiyo hadi tarehe 02.07.2012 kwa kidato cha pili, tatu, Nne na sita kwa kuwa imeonekana kuwa ndio viongozi wa uharibifu huo na wanafunzi wajapo shuleni hapo waje na wazazi wao na maelezo binafsi kwa barua.

Hadi mwandishi anaondoka hapo jeshi la polisi liliimarisha ulinzi shuleni hapo na wanfunzi 24 wamefikishwa police kwa mahojiano zaidi.Na mwandishi wetu Ally kingo Rungwe

2 comments:

mick nathan said...

ni mabadilko tu ya watanzania wanagoma leo kesho watagoma chuo hii ni kutokuwa makini kwa taasisi zetu inapendeza vijana tanzania ya leo bila kugoma, kuvunja bado

mick nathan said...

inapendeza vijana manake tz ya leo bila kugoma na kufanya matukio kama hayo watawala wanalala uzembe wa taasisi husika huo