Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, May 19, 2012

WAKAZI WAILALAMIKIA SERIKALI KUTOKANA NA KUSHINDWA KUDHIBITI VITENDO VYA UPIGAJI NONDO MKOANI MBEYA.
Bwana Oscar
Mbalamwezi (47) mkazi wa mtaa wa Chemchemi Kata ya Igawilo jijini
Mbeya aliyepigwa nondo majira ya saa saba usiku wakati akitoka
kuangalia mpira jana, akiwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa iliyopo
jijini hapa.(Picha na maktaba ya mtandao huu)
******
Habari na Yohana Katema, Mbeya.
Wakazi wa Kata ya Iyela Jijini Mbeya wameulalamikia uongozi wa Serikali ya mtaa, halmashauri na jeshi la polisi kushindwa kudhibiti vitendo vya upigaji nondo pamoja na kuboresha miundombinu ya elimu na barabara.

Baadhi ya wakazi wa kata hiyo Lusekelo Mwalukasa, Ipyana Malangalila na Yusuph Mwakafilwa wamesema mara kwa mara wamekuwa wakitoa malalamiko ya ujenzi wa barabara, vyumba vya madarasa vya shule ya sekondari ya kata pasipo mafanikio ya aina yoyote.

Aidha wamesema licha ya zaidi ya watu 6 kupingwa nondo katika kipindi kifupi hakuna jitihada zozote ambazo wameziona zikichukuliwa na uongozi wa kata katika kuwapata wahusika wa natukio hayo.

Kwa upande wake Afisa mtendaji wa Kata hiyo Ezekiel Kipako, amesema suala la uboreshaji wa barabara linaendelea, ambapo barabara yenye urefu wa kilometa moja na nusu itajengwa kwa kiwango cha lami na suala la upigaji nondo upelelezi unaendelea ili kuwabaini wahusika wa watukio hayo.

1 comment:

Mwangwitwa Chris said...

Jamani hivi kuna tatizo gani mkoani mbeya?mbona vitendo vya kupigana nondo vimeshamiri sana?wadau naomba mnisaidie tatizo ni nini?watu hawana huruma kiasi hicho?kila kukicha mbeya ni nondo tu,mimi ni mdau wa mkoa huo japo nimezaliwa nje ya mbeya nitabaki kuwa mimi ni wa hapo tu,tunaogopa hata likizo zetu kwenda mbeya imefikia hata watoto wetu wanatuuliza kwanini watu wanapigwa nondo mbeya hata kuwapa majibu mazuri tunashindwa ni aibu sana ndugu zangu kuendelea na tabia kama hii tubadilike ndugu zangu,watu bado wanaamini ili upate mali mpaka uende kwa waganga wa kienyezi wakupe masharti nenda kaue mtu kwa kupiga mtu nondo ndio upate utajiri si kweli ndugu zangu,utajiri wa namna hii hausidii,tumwogope MUNGU tuwe na hofu ya MUNGU naamini tutafanikiwa tu,MUNGU IBARIKI MBEYA NA WATU WAKE