Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, May 16, 2012

WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUFUATA MISINGI NA MAADILI YA UANDISHI WA HABARI MKOANI MBEYA.



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa
Abbas Kandoro katika picha ya pamoja na Waandishi wa habari mkoani
Mbeya, nje ya Ukumbi wa Itemba Village mara baada ya kumalizika kwa
Kongamano la Uhuru wa Vyombo vya habari.
******
Habari na Angelica Sullusi, Mbeya.

Waandishi wa habari Mkoani Mbeya wametakiwa kuandika habari
zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na zenye manufaa kwa wananchi na kuachana na
habari kutoka chanzo kimoja.


Hayo yameelezwa na Mwandishi wa habari Mkongwe nchini Phill
Karashani - katika semina iliyoandaliwa na Shirikisho la klabu za waandishi wa
habari Tanzania(UTPC) kwa waandishi wa Mkoani mbeya juu ya habari za uchunguzi.


Akitoa mada kwa wanahabari juu ya uandishi wa habari za
uchunguzi Karashani amesema kuwa wakati umefika kwa wanahabari kutumia taaluma
zao vyema kwa kujikita katika kuandika habari za uchokonozi zilizojificha
ambazo si rahisi mtu kuzitambua.


Jumla ya waandishi wa habari 20 kutoka vyombo mbalimbali
vya habari Mkoani hapa wanahudhuria mafunzo hayo ya siku sita ambapo Katibu
Tawala wa Mkoa huu Mariam Mtunguja aliyafungua mafunzo hayo juzi, Mei 14 mwaka huu.

No comments: