Mbunge wa Jimbo la Mbozi Magharibi Mheshimiwa David Silinde.
*Dr Siyame kulipa gharama za kesi.
*Kesi yaondolewa kabla ya hukumu.
*Miaka mitatu ya ushindi.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Jopo la majaji watatu wa mahakama ya Rufaa Mkoani Mbeya, wametupilia mbali rufaa ya Mbunge wa zamani wa Jimbo la Magharibi kwa tiketi ya CCM Dr Lucas Siyame ya kupinga matokeo ya Uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba mwaka huu dhidi ya Mbunge wa sasa mheshimiwa David Silinde wa tiketi ya CHADEMA.
Mheshimiwa Silinde alitetewa na wakili wa kujitegemea Bwana Benjamin Mwakaganda na Dr. Siyame alikuwa akitetewa na wakili Bwana Victor Mkumbe.
Kesi hiyo ambayo imesikilizwa na jopo la Majaji wa tatu wa mahakama ya rufaa, wakiongozwa na Jaji Msofe akisaidiana na Jaji Mbaruku.
Mapema Mei 2 mwaka huu katika mahakama hiyo ambayo ni ngazi ya juu kabisa, Wakili wa Dr. Siyame aliiambia mahakama kuwa wao kama walalamikaji wameamua kuiondoa kesi na hawako tayari kuendelea nayo na kwamba wako tayari kulipa gharama zote za kesi hiyo.
Awali keeshi hiyo ilitolewa hukumu mahakama kuu Julai mosi mwaka 2011, ambapo mahakama hiyo chini ya Jaji Wambura ilimpa ushindi Mbunge David Silinde, hivyo kumlazimu Dr, Siyame kukata rufaabkupinga hukumu hiyo, ambapo alidai kuwa Vituo vya kupigia kura vilizidishwa na pia kulikuwepo na kura hewa ambazo zilimpa ushindi Silinde katika majumuisho ya kura na pia fomu za matokeo hazikuwa halali.
Kesi hiyo iliyodumu kwa muda wa miezi 10 na kuisha Mei 2 mwaka huu, ilivuta watu wengi katika jengo la mahakama kuu Jijini Mbeya katika eneo la Forest.
Mheshimiwa Silinde kupitia wakili wake amesema ndani ya siku 60 wawe wamewasilisha madai ya gharama za kesi hiyo ili ziweze kupitiwa na wakili wa Dr. Siyame ili zilipwe.
Hata hivyo akionge nje ya mahakama Mbunge huyo amesema huo ni ushindi wake wa tatu mfululizo kupitia Uchaguzi mkuu ambapo Novemba 3 mwaka 2010 alitangazwa kuwa mshindi wa Jimbo la Mbozi Magharibi, na wa pili Julai mosi 2011 aliposhinda mahakama kuu na watatu ni Mei 2 mwaka huu katika mahakama ya rufaa na kuongeza kuwa kesi zote za CHADEMA zinazotolewa maamuzi kati ya Mei 1 mpaka 5 lazima ishinde.
No comments:
Post a Comment