Hii ndiyo barua iliyogushiwa |
“Hili ni kosa kubwa kwa mtu kuibuka na kutoa vitisho kwa kutumia majina ya viongozi wa juu na ofisi zao, kwani tumefanya uchunguzi wa barua hizo kwanza hazijafuata taratibu za serikali, lakini pia wahusika waliotajwa kutoa barua hiyo toka TAMISEMI wamekataa kuhusika tena kwa maandishi.” Alisema Kandoro.
Alitumia fursa hiyo kuonyesha na kugawa nakala za barua hiyo kwa waandishi wa habari, yenye kumbukumbu namba CAB.65/223/01/23 iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa TAMISEMI M.A Pawaga, ikiwa na baadhi ya maneno yanayosomeka . … “Kama ulivyoitilia mashaka barua hiyo na tathmini iliyofanywa ofisi hii hasa kwa kuzingatia saini ya mwandishi pamoja na mtiririko wa maudhui ya barua hii, tumegundua kuwa ni ya kughushi ,” ilifafanua sehemu ya barua hiyo
Akifafanua zaidi kuhusu zhilo Kandoro alisema hakuna sehemu wala kipengele kwenye sheria ya kahawa kinachozungumzia biashara ya kahawa mbichi, hivyo kitendo cha watu kutaka kulazimisha biashara hiyo ni makosa kisheria.
Hata hivyo Kandoro alipobanwa aeleze uchgunguzi wa awali umebaini mhusika aliyeandika barua hiyo, alisema suala hilo ni la kitaalamu na tayari rimeshafikishwa polisi wao ndio wanauwezo wa kumbaini mhusika na hatimaye kumkamata.
Wakati mkuu wa mkoa akitoa agizo hilo, kanda wa polisi mkoani hapa Advocate Nyombi alipoulizwa hatua zilizofikiwa alidai yuko likizo, lakini baadhi ya maofisa wa jeshi hilo ambao si wasemaji walilihaskikishia gazeti hili kuwa suala hilo lipo mikononi mwa polisi na linafanyiwa kazi
.
Hata hivyo hawakuwa tayari kueleza kama mhusika amekamatwa na kuwataka waandishi kuwa na subira ili uchunguzi ukamilike na hatua zitakazokuwa zimechukuliwa juu ya sakata hilo la kughushi nyaraka muhimu za serikali .
Sakata la ununuzi wa Kahawa mbichi wilayani Mbozi limekuwa la muda mrefu ambapo baadhi ya kampuni zilizopigwa marufuku na serikali ya mkoa kulalamika kuwa uamuzi huo ni wa kibabe kwa kuwa wao wananyaraka halali za serikali zinazowaruhusu kununua kahawa hiyo.
Miongoni mwa kampuni hizo ni Lima ltd , ambayo inadaiwa kughushi barua yenye kumbukumbu namba A.1 80/361/12/09,inayodaiwa kuandikwa na mmoja wa maofisa waandamizi kutoka ofisi ya Waziri mkuu aliyetajwa kwa jina la D. Bandisa,ikimtaka Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na uongozi wa wilaya ya Mbozi kuiruhusu kampuni hiyo kuendelea na ununuzi wa kahawa mbichiwilayani humo.
Lakini miaka miwili iliyoipita madiwani kutoka halmashauri zote zinazolima zao hilo zilipinga uuzaji wa kahawa mbichi kupitia vikao vya baraza la madiwani.
Habari kwa hisani ya Kenneth Ngelesi, Mbeya
Picha na Josep Mwaisango
Picha na Josep Mwaisango
No comments:
Post a Comment