Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, April 12, 2012

RAIA MBALIZI MBEYA WAMKATAA MWANAJESHI KUISHI NAE URAIANI



WANANCHI wa kitongoji cha Tazara kilichopo katika kijiji cha  Mbalizi mkoani Mbeya wamemtaka askari wa jeshi la wananchi (JWTZ) kikosi cha 44 Karume Camp, Chacha Mwita, ahame makazi yake na kurudi kambini kwa madai kuwa askari huyo amekuwa akitishia usalama wa wao kila kuchwapo.

Hayo waliyasema bayana katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tazara wiki iliyopita baada ya uongozi kuitisha mkutano huo ili kujadili mahusiano mabaya yaliyokuwepo baina ya askari huyo na raia anaoishi nao mtaani hapo.

Mkutano huo uliokuwa chini ya Mkuu wa upelelezi mkoa wa Mbeya Elias Mwita (RCO) ambaye alihudhuria baada ya kupokea malalamiko ofisini kwake kwamba hali ya usalama katika eneo hilo si shwari kutokana na msigano uliopo.

Mkuu huyo aliwaambia wananchi kuwa mapema mwezi huu alipokea ugeni ofisini kwake ulioongozwa na Mwanajeshi Chacha ukiimtuhumu Benson Mwakilembe (Tall) kwamba anawanyanyasa wananchi wa eneo hilo na kwamba wananchi waliowengi hawamtaki mwananchi huyo.

Alisema Chacha aliongozana na wenzake ambao aliwataja kwa majina kuwa ni Cosmas Maluli na Mchungaji wa kanisa la EAGT usharika wa Galilaya Ayub Mwasiposya ambao wote walikuwa wakimtuhumu Mwakilembe kuwa hana mahusiano mazuri na wananchi wa eneo hilo.

Mwita alisema baada ya kuelezwa hivyo aliona ni vema afike kuwasikiliza wakazi wote wa mtaa huo badala ya kuwasikiliza watu wachache waliofika ofisini kwake.

Mchungaji Mwasiposya alisimamishwa na kuwa wa kwanza kujieleza katika mkutano huo ambapo alikiri kufika ofisini kwa Mwita lakini kwa shinikizo la Chacha aliyemdanganya kwamba wakapatane na Mwakilembe kufuatia tofauti zao  hapo awali.

Mchungaji huyo alikanywa katika mkutano huo kutumia vizuri mahubiri yake ambayo baadhi ya wakazi wamekuwa wakiyalalamikia kwa madai kwamba amekuwa akiipotosha jamii kutokana na kuongelea habari za kishirikina ambazo aliwahi kuzielekeza kwa Mwakilembe na akakamatwa kwa kushindwa kuthibitisha kasha akasamehewa

Sababu zilizopelekea wananchi kumtaka mkuu wa upelelezi amhamishe Chacha kwenye mtaa huo mbali ya vitisho pia walidai kwamba ni mchochezi na anatumia vibaya kazi yake kwa raia kitendo ambacho walikifafanua kuwa analichafua jeshi hilo lenye heshima kubwa barani Afrika na dunia kwa ujumla.

Walisema amekuwa na tabia ya kuwapeleka watu katika kituo kidogo cha polisi cha Mbalizi bila makosa na kuzuia sungusungu kufanya kazi yake pia amewahi kuomba rushwa ya sh.100,000 ili kumwachia kijana mmoja ambaye alimtuhumu kumwibia kuku wawili madai ambayo walisema hayakuwa ya kweli.

Hata hivyo mkuu huyo wa upelelezi alisema kuwa mtanzania anahaki ya kuishi mahali popote kwa mujibu wa taratibu za serikali lakini pia alifafanua kuwa kwa kuwa Chacha ni mtumishi wa serikali atafanya mawasiliano na viongozi wake ili kuliweka sawa suala la kumtaka Chacha arudi kambini na akasema kuwa Chacha aache kutumia jina lake kutafuta umaarufu.

Tuhuma hizo zilitolewa katika mkutano huo ambao pia Chacha alipewa fursa ya kujieleza mbele ya mkuu wa upelelezi na alikiri kupeleka malalamiko hayo kwa mkuu huyo wa upelelezi kitendo ambacho kiliibua hasira kwa wananchi na kumtaka asiendelee kujieleza.

Awali Chacha ndiye aliyeuthibitishia mkutano kwa kumtuhumu kijana mmoja ambaye hakumtaja jina kwamba alimkamata akiwa na kuku wawili wa wizi lakini kauli hiyo ilimgeuka baada ya mama mmoja kusimama na kuueleza umma kuwa, malalamiko ya Chacha kuibiwa kuku  hayakuwa ya kweli kwani aliliunda tukio na kutumia vitisho vya uaskari ili kujipatia kiasi hicho cha pesa.


Kwa hisani ya Gordon Kalulunga, Mbeya

No comments: