Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Edward Ngoyai Lowassa ametoa shilingi milioni 10, kwa ajili ya ujenzi
wa Kanisa la EAGT lililopo Mji mdogo wa Tunduma, Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya.
Fedha hizo zimetolewa jana katika harambee ya
kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo, iliyofanyika katika viwanja vya Hoteli ya High
Class mjini humo.
Lowasa alitumia zaidi ya dakika 28 pekee kuwepo
kwenye viwanja hivyo ambapo amesema kuwa watanazania wanapaswa kuwa na wito wa
kujenga nyumba za kuabudu kuliko kujenga zaidi nyumba za starehe zikiwemo Bar.
Amesema kuwa amefurahi kualikwa katika harambee
hiyo na kwamba kwa sasa nchi ipo kwenye kipindi kigumu cha uchumi na masuala ya
katiba mpya, hivyo amewaomba wakristo kupanga ratiba ya kuiombea nchi ili
iendelee kuwa na amani na watanzania kuendelea kuimarisha ushirikiano na umoja
wa kitaifa uliopo nchini.
Aidha, amesema jambo hilo ni muhimu kwa kila
mtanzania akiliombea taifa, Tanzania haitaweza kutokea migogoro na vita za
wenyewe kwa wenyewe kama ilivyo kwa mataifa mengine mfano Nigeria.
Baada ya hotuba yake hiyo fupi aliwaita wasaidizi
wake jukwaani na kuwaagiza wampande na mfuko wa fedha na kisha akamkabidhi
mfuko wa pesa taslimu shilingiu milioni 10, Askofu Keneth Kasanga wa kanisa
hilo.
Kwa uapnde wake Askofu huyo alimshukuru Waziri
mstaafu Lowasa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Monduli kuwa amejenga nyumba ya
Mungu na hawezi kumuacha katika mambo yake yote na mahitaji pia.
Kanisa hilo lina zaidi ya waumini 750,
walipanga kuwa na kiasi cha shilingi milioni 750 na siku hiyo zimekusanywa
jumla ya shilingi milioni 17.9, huku fedha zilizoahidiwa ni shilingi milioni
Habari kwa hisani ya kamanga na Rashidi Mkwinda |
No comments:
Post a Comment