Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, April 3, 2012

BWANA HARUSI NDIYO CHANZO CHA KUTOFUNGWA HARUSI SI BI HARUSI KAMA ILIVYODAIWA


Ikupa akiwa na mchumba wake Gervas siku ya send off huko Mwakaleli

 
 Familia ya Bibi Harusi Ikupa Mwalukosya (29) katika picha ya pamoja nje ya nyumba yao siku moja baada ya harusi kutofungwa kutokana Ukata, uliopelekea Bwana harusi Mwalimu Gervas Shihamba Makambuya (29), kushindwa kutuma pesa kwa ajili ya nauli ya kumfirisha Bibi harusi pamoja na wapambe

Bibi harusi Ikupa Mwalukosya (kushoto) akiwa na Mchungaji Nelusigwe Ikuka Mwangosi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Jimbo la Mwakaleli, akimfariji bibi harusi baada ya bwana harusi kushindwa kutuma pesa kwa ajili ya usafiri.


Wazazi wa Ikupa Dkt Akimu Mwalukosya pamoja na mkewe wakiingia kwenye sherehe ya kumuaga binti yao

Ikupa akimkabidhi ua mchumba wake

Bwana harusi mtarajiwa akiwa nyumbani kwao huko sae Mbeya akisubiria familia hizi mbili kukutana na kujuwa hatma ya ndoa yao


Bwana harusi chanzo cha harusi kutofungwa kutokana na kutokuwa na mawasiliano mazuri na washenga wake ambao ni Bwana Amoni Mwangosi ambaye ni mshenga wa Bibi harusi na Bwana Angolile Mwakisilwa ambaye ni mshenga kwa upande wake wa Bwana harusi.

Bwana harusi alitumia watu wengine kupeleka nauli ya sh 24,000/= ya kumchukua bi harusi na mpambe wake bila kufuata taratibu za kimira za kuwajulisha washenga wake ndiyo waende kumchukua mchumba wake hata hiyo watu hao walikataliwa kwa kutotambuliwa na familia hiyo ya bi harusi na kutaka wahusika wafike ili wakabidhiane kwa taratibu zinazotambulikana

 
Kwa upande wake wa Mzazi wa Bibi harusi Mzee Akimu Mwalukosya, amesema hana kinyongo bali yaliyopita si ndwele na wagange yajayo kwani makosa yaliyofanyika yanazungumzika.

Leo jioni kamati ya maandalizi upande wa bwana harusi wanakutana kujadili swala hilo


Hata hivyo kamati ya sherehe ya bwana harusi itakutana kesho(jumatano) kupata hatima ya harusi hiyo.1 comment:

Anonymous said...

Mila hizi zilifaa enzi hizo hakuna magari. Watu walikuwa wanatembea kwa miguu. Sasa kwakuwa mila haziendi na wakati matokeo yake ndo haya!