Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini(CHADEMA), mheshimiwa Joseph Mbilinyi.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi amewataka wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo ya Elimu Jimboni humo kuchangia mfuko maalumu wa elimu ambao utatumika kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo kwa kukosa fedha za kulipa ada.
Ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara na wakazi wa Kata ya Isanga uliofanyika kwenye viwanja vya Ilolo ambapo amesema uamuzi wa kuanzishwa kwa mfuko huo umetokana na wananchi wengi kufika ofisini kwake kuomba msaada wa kusomeshewa watoto wao.
Ametaja jina la mfuko huo kuwa ni Mbeya Educational Trust Fund na ulianzishwa mwaka jana na tangu uanzishwe zaidi ya shilingi laki nne na elfu themanini ambazo zimepaikana huku wadau wakiaidi zaidi ya shilingi milioni nane.
Aidha,amewataharisha wazazi kuwa kukosekana kwa ada kwa baadhi ya wanafunzi kunawakosesha viongozi bora kwa kuwa viongozi waadilifu siku zote hutokea katika familia masikini ambao wakipewa elimu ndio wenye uwezo mkubwa.
Pia,Mbunge huyo amesema kuwa mfuko huo ameuanzisha yeye kwa manufaa ya wananchi wa Jimbo zima na utasimamiwa na viongozi watakaochaguliwa na wananchi wenyewe hivyo hautakuwa na itikadi yoyote ya chama bali kwa ustawi na maendeleo ya jimbo hilo.
Mbunge huyo amesema kuwa mfuko huo uliozindulia mwishoni mwa mwaka jana una shilingi 480,000 pamoja na shilingi 8,000,000 zilizoahidiwa na wadau mbalimbali,unatarajiwa kuanza kufanya kazi mapema mwezi aprili mwaka huu mara baada ya usajili kukamilika.
Habari na Angelica Sullusi, Mbeya
|
No comments:
Post a Comment