Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, February 27, 2012

WANUSURIKA KIFO WAKIMSINDIKIZA MAKAMU WA RAIS DKT BILAL

MBUNGE wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mbeya,Hilda Ngoye 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Beatha Swai 

MBUNGE wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mbeya,Hilda Ngoye na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Beatha Swai wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwamo kugonga pikipiki na kisha kupinduka mtaroni.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa nne asubuhi katika mji wa Chimala wilaya ya Mbarali ambapo msafara wa katibu huyo pamoja na mbunge walitangulia mbele kabla ya msafara wa makamu wa raisi kuanza.
Ajali hiyo ilihusisha gari lenye namba za usajili STK 2429 analotumia katibu tawala wa mkoa Mbeya na pikipiki ambayo namba zake hazikupatikana maramoja pamoja na jina la mwendesha pikipiki huyo.
Katika eneo la tukio kamanda wa polisi mkoani hapa Advocate Nyombi alisema viongozi hao hawakujeruhiwa isipokuwa mwendesha pikipiki ambaye alikimbizwa katika hospitali ya misheni ya Chimala kwa ajili ya matibabu.
Aidha chanzo cha ajali alisema ni mwendesha pikipiki kugeuza katikati ya barabara wakati gari la katibu huyo likiwa karibu naye hiyo dereva alishinwa kulimudu gari lake kisha kutumbukia katika ukingo wa barabara.



No comments: