Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, February 8, 2012

NMB MBEYA YATOA MSAADA WA MADAWATI 110 KWA SHULE ZA MSINGI NNE JIJINI MBEYA

Akikabidhi msaada huo wa madawati meneja wa Benki ya NMB kanda ya nyanda za juu kusini Bi.Lukesia Bena amesema benki yake imetoa msaada huo baada ya kuridhia ombi lililotolewa na mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi kwa benki hiyo kusaidia madawati kwa shule za msingi ili kuwajengea uwezo wanafunzi kupenda masomo
Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imetoa msaada wa madawati mia moja na kumi  kwa shule za msingi Sinde, Maanga, Lyoto na Ilomba ili kuboresha huduma za elimu kwa shule hizo.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya mkurugenzi wa jiji la Mbeya Afisa elimu wa shule za msingi jiji Bi.Aurelia Luensi ametoa shukrani kwa uongozi wa Benki hiyo kuchangia katika elimu na kuwasihi walimu na wanafunzi kuyatunza madawati hayo

No comments: