Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, February 9, 2012

MCHUNGAJI AKUTWA AKIWANGA , AFANYA MAOMBI KWA KUWASHIKA WANAWAKE SEHEMU ZA SIRI NA MATITI - MBEYA


Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mchungaji Geofrey Joram wa Kanisa la Restoration Bible Church (RBC) lililopo Inyala jijini Mbeya amekutwa akiwanga katika nyumba ya Bwana Amanyisye Fungo ambaye anaishi jirani na kanisa hilo.

Tukio hilo limetokea majira ya saa kumi na mbili asubuhi Februari 8, mwaka huu Mchungaji huyo akiwa na baadhi ya waumi wake ambao idadi yake haikuweza kufahamika alikutwa akiwa ameshika chupa iliyodaiwa kuwa na dawa ya kienyeji nakuinyunyiza katika mlangoni na chumba ambacho analala Bwana Amanyisye.

Licha ya kutenda tukio hilo mchungaji huyo alifumwa na watoto wa Bwana Amanyisye ambao wamefahamika kwa jina la Baraka Amanyisye (18), mwanafunzi wa kidato cha tatu na Eliud Amanyisye (19) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Lupeta ambao walikuwa wakielekea shuleni kwao.

Watoto hao walipomhoji Mchungaji huyo kwanini anatenda tukio hilo, ndipo mchungaji huyo kuja juu na kupiga kelele hali iliyompelekea baba wa watoto hao Bwana Amanyisye kuamka, ili kujua nini kilichotokea na kisha kuwakuta waumini na mchungaji huyo akiwa na chupa mkononi, ambapo aliitwa balozi wa mtaa huo Bwana Frenk Mwambagi.

Balozi huyo wa mtaa Bwana Mwambagi alipomuuliza mtuhumiwa huyo kulikoni mchungaji alishindwa kujibu na ambapo balozi huyo aliamua kwenda kwa Mwenyekiti wa mtaa Bwana Nelson Mahena kutoa taarifa na mtendaji wa mtaa Bi Christina Atakwani ambao walienda kutoa taarifa Kituo cha Polisi cha Iyunga jijini Mbeya.

Hata hivyo Mchungaji huyo alikimbia kusikojulikana, ambapo hata kwake hakuweza kupatikana na waumini wake kutawanyika mara baada ya Viongozi wa serikali ya mtaa kwenda kutoa taarifa kwa Jeshi la polisi Kituo cha Iyunga.

Imedaiwa kuwa mtuhumiwa amekuwa akilalamikiwa kutokana na imani hizo za kishirikina kutokana na kuwashika wanawake sehemu za siri na  matiti wakati akiwafanyia maombezi, na taarifa za uchafu huo zilipelekwa katika uongozi wa mtaa na kumuonya zaidi ya mara tatu lakini alikaidi na kikao cha mwisho cha onyo kilifanyika Februari 2, mwaka huu mbele ya Askofu wake Mkuu Emmanuel Tumwidike, ambapo mchungaji huyo alikiri na kuahidi kumwamisha kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni kukiuka maadili ya kanisa hilo.

Wakati huohuo wakati Askofu Tumwidike akifanya  jitihada za kumuhamisha zikifanyika ndipo mchungaji huyo alipokutwa na tukio hilo na kwamba atalishughulikia leo lakini Uongozi wa Serikali katika mtaa huo uchukue hatua za kisheria.

Mpaka habari hii inaandikwa mchungaji huyo hajaweza kupatikana licha ya wananchi kufanya msako mkali.

1 comment:

Anonymous said...

aaa bana mwandishi mchungaji kakimbia sawa, vipi umeshindwa hata kumuhoji mwanamke mmoja akazungumza japo kidogo,

usikimbilie kuweka habari isome kwanza kwa umakini. Imewanyima haki hao lazima wanawake wenzao wanajua wangekuambia bana