Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, February 9, 2012

Benki ya EXIM yatoa mkono wa pole kwa waathirika wa soko la Sido Mbeya

Meneja wa Benki ya Exim, tawi la Mbeya Bw. Geoffrey Kitundu (kushoto), akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe. Evance Balama, (kulia) hundi ya shilingi milioni 13,350,000/= fedha ambazo zimetolewa na benki hiyo kama mkono wa pole kwa akina mama wafanyabiashara katika soko la SIDO, la jijini Mbeya ambalo liliungua na kuteketea mwishoni mwa mwaka jana. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa soko hilo, Bw. Wilson Mwakisilwa.

Baadhi ya akina mama walioathiriwa na ajali ya moto katika soko la SIDO jijini Mbeya, wakiwa wamenyanyua juu hundi ya shilingi milioni 13,350,000/=, muda mfupi baada ya kukabidhiwa hundi hiyo na mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Evance Balama (wa tatu kutoka kushoto), muda mfupi baada ya Mkuu wa Wilaya kupokea hundi hiyo toka kwa meneja wa Exim Bank, tawi la Mbeya Bw. Geoffrey Kitundu (wa kwanza kushoto)



HATIMAYE Benki ya Exim tawi la Mbeya imetimiza ahadi ya kuwapatia wanawake wafanyabiashara 267 walioathiriwa na moto uliyounguza bidhaa zao katika soko la SIDO kwa kitita cha shilingi milioni 13.3 ili kuendeleza biashara zao kwa matumaini zaidi.

Meneja wa tawi la benki hiyo Geoffrey Kitundu wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada huo alisema benki yake ilipokea kwa mshituko taarifa za kuungua kwa Soko hilo na kulazimika kufikiria jinsi ya kuwasaidia wanawake walioathirika.

“Tulipokea taarifa za kuungua kwa Soko la Sido kwa masikitiko makubwa. Leo tunatimiza ahadi tuliyoitoa kwa waathirika na nimatumaini yetu kuwa itasaidia kuwasogeza mbele kidogo waathirika wa janga la moto pamoja na familia zao,” alisema Kitundu.

Kitundu alisema benki yake inampango maalum wa kumkomboa mwanamke kwa kutambua mchango wake mkubwa wakuinua uchumi wa taifa.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Evans Balama katika hafla hiyo aliushukuru uongozi wa benki hiyo kwa kutimiza ahadi ya kusaidia ahadi wafanyabiashara hao na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano huo.

“Desemba mwaka jana nilikuja kutembelea Soko la Sido baada ya kupata taarifa kuwa limeungua. Katika soko hilo nilikutana na watalaam wa benki ya Exim ambao waliahidi kusaidia.

“Tunashukuru benki ya Exim kwa kutimiza ahadi yao leo. Nimatumaini yetu kuwa fedha hizi zitasaidia kuwasogeza waathirika hatua moja mbele. Nawahasa wanawake kuzitumia fedha hizi vizuri kuendeleza biashara zao na si vinginevyo,” alisema Balama.

Balama aliwasii wanawake hao kukopa na kurejesha mikopo yao kwa haraka iwezekanavyo ilikuendeleza biashara zao.


“Msiogope kukopa fedha benki. Bahati nzuri tumeshapata benki ambayo imeonyesha ushirikiano. Ombi langu kwenu ni kuhakikisha mnatumia mikopo hii kwa malengo ya kuboresha biashara zenu,” 


No comments: