Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, February 18, 2012

JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LAWAMANI KUHUSIKA NA KIFO CHA MWANACHUO ALIYE FARIKI SIKU YA WAPENDANAO YANI VALENTINE DAY



Marehemu Daniel Godluck Mwakyusa (31) ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha TEKU aliyeuawa na Askari wa Jeshi la Polisi PC Maduhu tarehe 14/02/2012 katika sikukuu ya wapendanao {valentine day].
Baadhi ya majeraha ya majeraha yaliyotokana na kipigo katika mwili wa marehemu Daniel Godluck Mwakyusa (31) ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho aliuawa na Askari wa Jeshi la Polisi PC Maduhu tarehe 14/02/2012 katika sikukuu ya wapendanao {valentine day].
Baadhi ya majeraha yaliyoyokana na kipigo atika mwili wa marehemu Daniel Godluck Mwakyusa (31) ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho aliuawa na Askari wa Jeshi la Polisi PC Maduhu tarehe 14/02/2012 katika sikukuu ya wapendanao {valentine day].
******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Watu watatu wamefariki dunia mkoani MBEYA katika matukio matatu tofauti, likiwemo la tukio la Mwanafunzi wa chuo kikuu cha TEKU kilichopo jijini mbeya marehemu Daniel Godluck Mwakyusa (31) ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho aliuawa na Askari wa Jeshi la Polisi PC Maduhu tarehe 14/02/2012 katika sikukuu ya wapendanao {valentine day].

Marehemu akiwa na wenzake wanne walikuwa katika matembezi ambapo polisi walikuwa doria walikuta vijana hao wakipata vinywaji ndipo waliwatuhumu kuwa ni majambazi ambapo PC Maduhu alimpiga marehemu risasi mbili kwa kutumia bunduki aina ya [SMG].

Pia marehemu aliporwa shilingi laki tatu pamoja na simu ya mkononi .

Kwa mujibu wa baba mzazi wa marehemu huyo Bwana Pastory Mwakyusa amesema kuwa anasikitishwa sana na kitendo hicho kilichotokea kwani mwanawe hakuwa na tabia ya wizi au ujambazi hivyo ameliomba Jeshi la Polisi kueleza sababu ya kumuua mtoto wake.

Hata hivyo Jeshi la Polisi lilitoa usafiri wa gari lenye nambari za usajili T 138 AFK aina ya Coster kwa ajili ya kusafirisha Mwili wa marehemu kwenda katika wilaya ya Kyela kwa ajili ya mazishi baada ya uchunguzi wa daktari kuthibitisha kuwa marehemu ameuwawa kwa risasi.

Tukio la pili marehemu Zuberi Mwajeleba (21) mkazi wa kijiji cha Ibumba wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya ambaye alinyongwa kisha mwili wake kutupwa katika mto wa Kanyegele wilayani humo.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amesema chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika na Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo.

Katika tukio la tatu limetokea majira ya saa nane mchana katika eneo la Ilomba jijini Mbeya ambapo pikipiki yenye namba za usajili T 834 BOX aina ya Shinray ambayo dereva wake bado hajafahika alimgonga mtoto Mildred Immanuel (10) mkazi wa eneo hilo.

Hata hivyo dereva alitoroka na kuitelekeza pikipiki katika eneo la tukio na pikipiki hiyo imehifadhiwa katika Kituo cha kati cha Jeshi la Polisi, na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya na Polisi wanafanya juhudi za kumtafuta dereva huyo.

HABARI YA KUFUFUKA.
Wakati huo huo katika hali isiokuwa ya kawaida Roza Simbeye ambaye ni mama wa mtoto mmoja katika kitongoji cha Isandula, kijiji cha Vuwile, Kata ya Isandula, aliyefariki Februari 16 majira ya saa kumi na mbili za jioni amefufuka wakati taratibu zote za mazishi zipokamilika kama kuchimba kaburi na kuchonga jeneza na taratibu za ibada.

Na ilipofika majira ya saa 3:30 asubuhi ya Februari 17 baada ya kaburi kuchimbwa na jeneza kukamilika zilianza taratibu za kuchukua mwili wa marehemu Roza chumbani ndipo watu waliopewa jukumu la kumwosha walishangaa kumwona marehemu akiwa hai huku akiwa amtoa macho kama vile mtu ametoka usingizini ambapo mpaka sasa kaburi halijafukiwa wala jeneza halijatumiwa na kufanya wanakijiji kubaki na mshangao.

5 comments:

Anonymous said...

Hii kali Ndo polisi wetu hao. Dah! inasikitisha sana watu waliopewa dhamana ya kulinda usalama ndo wanatugeuka Taifa linapotea vifo vya jinsi ni uozo kabisa. Haya wacha tuone mwisho wake.

Anonymous said...

gud informations,nimevutiwa na picha kuhusiana na mwanafunzi wa TEKU,naiomba jeshi la polisi kufuatilia kwa makini na kama ni uzembe askari huyo achukuliwe hatua kali..matukio na picha yanatufanya sisi wasomaji kuwa na uelewa kuhusu habari..kazi njema

Anonymous said...

POLENI NA MSIBA WA MWANCHUO MWAKYUSA NA WENGINE.NASHAURI POLISI KUWA MAKINI WAKATI WA DORIA VINGINEVYO WATAONEKANA KUTUMIA SILAHA VIBAYA NA JESHI LA POLISI KUPAKWA MATOPE

Anonymous said...

polisi mnaonyesha mfano gani kwa raia wengine kama ninyi mmeweza ku take action ya kuua mtu asiye hatia na kwanini kama mliona ni mwenye makosa msimpeleke kituo cha polisi ili kufuatilia na mjue je yeye ni nani na anafanya nini. jeshi la police muliangalie nyie mue kama example kwa watu wengine lakini mnaonyesha nidhamu mbaya. lakini jueni kwamba uhai wa mtu mmeupoteza na damu yake itawalalamikia milele.

Anonymous said...

inasikitisha sana,poleni sana wanambeya wenzangu.