Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, February 11, 2012

HALI HII NI NDOTO KUPUNGUA KWA AJARI ZA BARABARANI MKOANI MBEYA, ASKARI USALAMA WA BARABARANI WAFUMBIA SUALA HILI?

 Licha ya Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi, kuzuia magari ya mizigo maarufu kama Malori kubeba abiria, hali imekuwa tete kutokana na Askari wa usalama wa barabarani Kituo cha Mlowo, barabara ya Mlowo/Kamsamba wamekuwa wakiruhusu magari hayo kupakia abiria kupita kiasi kama inavyoonekana pichani. Mbali na askari hao kufanya ukaguzi hali hii imekuwa ikifanyika kila siku majira ya asubuhi na mchana. 

Mtandao huu umeshuhudia gari hii ya mizigo ikiwa imebeba abiria na mizigo kama baiskeli, vinywaji ikiondoka kutoka Mlowo kuelekea Kamsamba wilaya ya Mbozi, licha ya kukaguliwa na Askari wa usalama wa barabarani na kuruhusiwa kuondoka, ambapo kwa hali hii inatishia usalama wa abiria. (Picha zote na Ezekiel Kamanga, Mbozi).

No comments: