Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, January 27, 2012

AZRA VUYO JACK MTOTO ALIYEZALIWA MAHABUSU NA ANAENDELEA KUKULIA MAHABUSU WAZAZI WAKE WATUHUMIWA KUKUTWA NA MADAWA YA KULEVYA

MTOTO AZRA VUYO JACK AKIWA AMELALA

AZRA AKIWA AMEPAKATWA NA BABA YAKE VUYO JACK NJE YA MAHABUSU YA MAHAKAMA KUU MBEYA

BABA NA MAMA AZRA WAKIWA NA MTOTO WAO WAKISUBIRI KUINGIA MAHAKAMANI JANA ASUBUHI

ANASTAZIA CLOETE MAMA WA AZRA AKIFURAHI  BAADA YA JOSEPH MWAISANGO WA MBEYA YETU KUMWAMBIA KWA UTANI KUWA ATAMCHUMBIA AZRA ILI ABAKI MBEYA


WAKIWA NA NYUSO ZA FURAHA BAADA YA UTANI WA HAPA NAPALE  NJE YA MAHABUSU YA MAHAKAMA KUU MBEYA

MSAMARIA MWEMA EMILY MWAITUKA NDIYE ALIYEJITOLEA KUMHUDUMIA MTOTO AZRA HUKO MAHABUSU KWA KUMPELEKEA MAZIWA KILA SIKU



HILI NDILO GARI LA WAZAZI WA AZRA 




Wakati Tanzania ikiwa imeridhia mkataba wa kimataifa wa kutekeleza na kulinda haki za watoto na kusimamia kwa karibu ulinzi wa haki za binadamu, sasa serikali ina kila sababu ya kuangalia haki za watoto walioko gerezani kwa makosa ya wazazi wao.
  Miongoni mwa haki ambazo serikali inapaswa kuchunguza kwa undani na kubainisha kisa kilichosababisha mtoto mdogo wa kike wa miezi sita , Azra Vuyo Jack, ajikute yeye na wazazi wake wakiwa katika mahabusu ya gereza la Ruanda jijini Mbeya wakikabiliwa na tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya.
  Azra ambaye kwa jina la utani, kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Mbeya yetu huko gerezani anaitwa Merryciana au bibi jela jina ambalo limezoeleka zaidi mbali ya jina lake halisi alilopewa na wazazi wake la Azra   .
   Mtoto huyo wa kike aliendelea kukua katika tumbo la mama yake akiwa gerezani, hatimaye alizaliwa salama Julai 15 mwaka jana katika hospitali ya wazazi meta.
  Mama yake ni Anastazia Cloete (27) mwenye asili ya kizungu, raia wa Afrika ya kusini
  Cloete alikamatwa mwaka juzi, Novemba katika mpaka wa Tanzania na Zambia , mji mdogo wa Tunduma akiwa mjamzito na kutupwa mahabusu katika gereza hilo hali iliyomfanya aendelee  kulea ujauzito wake.
  Uchunguzi wa kina uliendelea kufanywa na madaktari wa hospitali hiyo hadi alipojifungua salama.
   Uchunguzi wa tukio la mtoto huyo hadi sasa umezusha mwendelezo wa harakati za kihabari na wanaharakati wa haki za binadamu kuona umuhimu wa kuondolewa kwa mtoto huyo ambaye kwa muda wote tangu azaliwe amekuwa akitumia maziwa ya kopo na hanyonyeshwi na mama yake mzazi.
  Mmoja wa ya wasamaria wema aliyejitolea kuwahudumia watuhumiwa hao waliyokumbwa na tuhuma za kukutwa na dawa hizo ni Emily Mwaituka ambaye amekuwa akifanya kazi kubwa ili kuhakikisha mtpto anakuwa na afya nzuri kwa kununuliwa makopo mawili ya maziwa kila wiki tangu alipozaliwa julai, mwaka jana.
  Mwaituka anasema amekuwa akinunua kopo moja la maziwa ya unga aina ya SMA 1 ambalo huuzwa sh 26000 na anapaswa kununua makopo mawili ili kuweza kumudu mahitaji ya mtoto huyo wa kike ambaye hanyonyi maziwa ya mama yake mzazi anayesubiri hatima ya kesi inayomkabili akiendelea kuwa mahabusu kwenye gereza la Ruanda jijini Mbeya.
  Uchunguzi uliofanywa na Mbeya yetu  umegundua kuwa Cloete aliyekuwa akisoma nchini kwao katika chuo cha Capetech alijifungua mtoto wa kike miezi sita iliyopita baada ya kushikwa uchungu akiwa mahabusu na kukimbizwa hospitali ya wazazi ya meta.
  Cloete ambaye amekuwa akitumia majina mawili kwani alipolazwa katika hospitali hiyo aliandikishwa jina la Anastazia Elizabeth wakati alifikishwa hospitalini hapo kwa uchunguzi akiwa mjamzito Januari 14 mwaka jana na kufunguliwa jarada la matibabu lenye namba 46 – 26 – 83.
  Uchunguzi umebaini kuwa raia huyo wa afrika ya kusini na mumewe , Vuyo Jack ( 31 ) waliokamatwa mpakani hapo, aligundulika kuwa mjamzito alipokuwa mahabusu na kuanza kupatiwa matibabu sahihi yaliyosaidia ujauzito wake kukua vizuri.
  Habari za ndani zinadai kuwa kwa muda wote huo baada ya ujauzito wake kugundulika alikuwa akipatiwa matibabu chini ya uangalizi wa madaktari na alipofikia  hatua za mwisho mjadala mzito ulifanywa na jopo la madaktari walioonyesha mashaka kuwa asingeweza kujifungua kwa njia ya kawaida na kutakiwa afanyiwe upasuaji.
 Imeelezwa kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake katika hospitali hiyo Peter Msafiri , alipofanya uchunguzi alibaini kuwa raia huyo hapaswi kufanyiwa upasuaji kwa vile alikuwa na uwezo wa kujifungua bila matatizo.
  Dk Msafiri alipohojiwa anasema Cloete alijifungua salama ingawa walitaka kumfanyia upasuaji lakini alipinga hatua hiyo na kudai kuwa anaweza kujifungua salama kwa njia ya kawaida.
  Baadhi ya wauguzi wa hospitali hiyo ambao hawakutaka majina yao kutajwa walidai kuwa raia huyo wa Afrika ya Kusini alijifungua mtoto wa kike na kwamba mama yake akiwa mahabusu amekataa kumyonyesha kwa madai kuwa hapati mlo wa kutosha unaomuwezesha kutoa maziwa ya kutosha kwa ajili ya mwanae.
  Cloete alilazwa hapo kwa ajili ya uchunguzi , hamnyonyeshi mtoto wake, kweli amejifungua mtoto mzuri wa kike, amesema kuwa hawezi kumnyonyesha na  anamlisha maziwa ya kopo akidai kuwa akinyonyesha atakosa nguvu kwa kuwa mahabusu alikowekwa hapati lishe bora anadai muuguzi mmoja.
 Miongoni mwa wanaharakati wa haki za binadamu walioguswa na habari za mtoto huyo kuendelea kukaa mahabusu na mama yake kulimgusa. Mchungaji William Mwamalanga, anasema kuwa kitendo cha mtoto huyo kuishi katika mazingira hayo hakuendani na haki za binadamu ambazo Tanzania imeridhia kwenye umoja wa mataifa.
  Mwamalanga anasema yeye na wanaharakati wenzake wanaandaa mpango maalumu wa kupigania haki ya mtoto huyo na kuhakikisha kuwa anaondolewa mahabusu baada ya kubainika kuwa amekuwa hanyonyeshwi na mama yake mzazi tangu alipozaliwa kwa madai kuwa hawezi kumnyonyesha kutokana na lishe duni anayopata akiwa mahabusu.
  Nakushukuru sana kuzisoma taarifa hizi, tunajiandaa ili kuona njia sahihi inayoweza kutusaidia kumtoa mtoto huyo mahabusu na kuiomba serikali iangalie kwa undani shauri hili kupitia kwa mwendesha mashtaka mkuu wa serikali ili kujua haki na stahili za mtoto huyo mchanga vinginevyo tunakiuka haki za watoto na binadamu ambazo Tanzania imeridhia kuzitekeleza, anasema Mwamalanga.
  Kumbukumbu za tukio hilo tulizonazo zinaonyesha kuwa raia hao wawili wa Afrika ya Kusini, waliokuwa wakiishi mtaa wa 2A Valley Road – Schaapkraal – Capetown walikamatwa na kilo 42 .5 za dawa za kulevya Novemba 18 mwaka juzi katika mpaka wa Tunduma na kufunguliwa – jalada namba TDM/IR/1763/2010.
  Katika tukio hilo ambalo Vuyo na Cloete walinaswa na dawa hizo walizozificha kwenye gari aina ya Nissana Hard body yenye namba za usajili CA – 508 – 656 lililokuwa likimilikiwa na Vuyo Jack waliokuwa wakitokea mkoani Morogoro kuelekea Afrika ya Kusini, Cloete alikuwa akisoma katika chuo cha Capetech.
  Kwa mujibu wa taarifa za ndani ambazo zimethibitishwa na Mkemia Mkuu wa Serikali dawa hizo za kulevya ni paketi 26 za cocaine zenye uzito wa kilo 28.5 paketi tatu za Heroine zenye uzito wa kilo 3.25 na paketi nane aina ya Morphine zenye uzito wa kilo 3.25, madawa hayo yote yanathamani ya zaidi ya sh bilioni 1.2.


picha na mbeya yetu


Habari na Christopher Nyanyembe

3 comments:

Anonymous said...

Dah kweli mtoto atolewe inshu hapa mtoto atolewe lupango....kwasaabu lupango mtoto anaweza kupata magonjwa mengi kwani kinga yake bado haijakomaa,pili mahabusu siyo sehemu inayofaa kumkuza mtoto kama kesi ya wazazi wake inachukua miaka mingi huyo mtoto huko jela atajifunza nini?

ALLY SHAABAN MGIDO'S 24 SEVEN 365 "HARAKATI HAZIKOMI" said...

kweli hili ni tatizo haswa na inahitaji ufunbuzi.Hivi inakuwaje mtoto kama huyo aendelee kuishi humo hahali ya kuwa inajulikana maisha ya lupango jinsi yalivyo magumu magonjwa mengi ya mipuko yanaweza yakampata mtoto.
Suala lingine huduma za mtoto huko jela je zinapatikana? sijui kama suala hili la mtoto kukaa nae lupango linaruhusiwa katika sheria na haki za kibinadamu.
Na lingine mtoto kukaa huko kama aivyosema mwenzangu anajifunza nini? Hivi wahusika hawaoni kama hili tatizo linahitaji ufumbuzi au? ni hayo tu.

tz biashara said...

Ni aibu kubwa kwa nchi yetu ambayo inaonekana wazi sheria na haki za kibinaadamu zinakiukwa.Kwanza polisi wanatakiwa wawe na kitengo maalum ambacho kiwe kinawasiliana na ustawi wa jamii ili kuepukana na matatizo ya kuhusiana na watoto ktk jela.Yaani hapa polisi wamemuonea sana huyu mtoto kumfungia jela kwa kosa la wazazi wake.