Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, November 14, 2011

ZAIDI YA WATOTO 1,000 WAMEJITOKEZA KUPEWA MATONE YA CHANJO YA MAGONJWA YANAYOWAKABILI WATOTO MTAA WA MWANYANJE, IGAWILO - MBEYA


Baadhi ya watoto kati ya elfu moja waliojitokeza jana kupatiwa matone ya chanjo ya kitaifa ambayo imetolewa na kitengo cha Afya kutoka Halmashauri ya jiji dhidi ya magonjwa ya Surua, Kupooza na Minyoo katika mtaa wa Mwanyanje, kata ya Igawilo jijini Mbeya.
Bi Foibe Fubile(kushoto), Bi Tulasiwona Fungo(katikati) na Bi Chelina Lusuva(kulia) kutoka Kitengo cha Afya katika Halimashauri ya jiji wakiendelea kutoa matone ya chanjo ya kitaifa dhidi ya magonjwa ya Surua, Kupooza na Minyoo kwa watoto katika mtaa wa Mwanyanje, kata ya Igawilo jiji Mbeya.
Afisa wa Afya halmashauri ya jiji la Mbeya Bwana Uswege Msomba(aliyevalia kofia kushoto) akiwa na Mtendaji wa mtaa wa Mwanyanje Bwana William Muhongole akipewa maelezo baada ya dawa kuisha kutokana na wingi wa watoto waliofika kupewa matone ya chanjo ya magonjwa ya Surua, Kupooza na Minyoo mtaani kwake.

1 comment:

Anonymous said...

tunaomba picha za mh mbunge wetu wa arusha mjini alivyopokelewa leo baada ya kauchiwa