Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, November 18, 2011

RAIS JAKAYA KIKWETE AKIONGEA NA WAZEE WA DAR ES SALAAM KWENYE UKUMBI WA (PTA)



Rais
Jakaya Kikwete akiongea na wazee wa mkoa wa Dar es salaam hivi jioni
hii kwenye ukumbi wa PTA viwanja vya maonyesho vya Mwalimu J.K.Nyerere
barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam. Rais Kikwete anazungumzia
masuala mbalimbali yakiwemo mamasuala ya kiuchumi na masuala ya mchakato
wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania








Wazee mbalimbali wa
chama na wastaafu wamekusanyika katika ukumbi huo ili kusikiliza na
ambapo mambo mbalimbali watakayoambiwa,ili nao pia waweze kufikisha
ujumbe kwa wanzao ambao hawajapata nafasi ya kuhudhuria katika mkutano
huo na wananchi kwa ujumla



Rais
Jakaya Kikwete akiwasilia kwenye ukumbi wa PTA tayari kuongea na wazee
wa Dar es salaam pamoja na wananchi kwa ujumla, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa
Dare salaam Meck Sadick na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es
salaam.




Rais
Jakaya Kikwete akiongoza viongozi wa mbalimbali na wazee wa Mkoa wa Dar
es salaam kumkumbuka mmoja wa wazee wa CCM ambaye alikuwa kiongozi
katika baraza la wazee katika picha kutoka kulia ni Mzee Kingunge
Ngombale Mwiru, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Meck Sadick na kutoka
kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam John Guninita na
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Dar es salaam Brigedia Mstaafu Hashim
Mbita.



Kutoka
kulia ni Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar
es salaam John Guninita katikati na Mkuu wa wilaya Mstaafu mama Hawa
Ngulume wakijadiliana jambo kabla ya Rais kuwasili katika ukumbi huo



Wazee mbalimbali wakiwa wamekusanyika kwenye ukumbi wa PTA tayari kwa kumsikiliza Mh. Rais Jakaya Kikwete.



Hapa wakionekana kujadiliana mambo kadhaa kabla ya Rais kuwasilia katika mkutano huo jioni hii.
Baadhi ya wazee kutoka mtoni Wilayani Temeke wakiwa katika ukumbi huo kwa ajili ya kumsikiliza Mh. Rais Jakaya Kikwete.



Picha Zote Na John Bukuku - Full Shangwe Blogu

No comments: