Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya picha Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge wa Tanzania wa kupambana na Ukimwi (TAPAC), Lediana Mng’ong’o, kwa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia umoja huo, wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Umoja huo tangu ulipoanzishwa. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma leo Novemba 18, 2011. Kulia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda
Picha ya pamoja
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiinua Mshumaa juu baada ya kuuwasha ikiwa ni ishala ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Umoja wa Wabunge wa Tanzania wa kupambana na Ukimwi (TAPAC), uliofanyika kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma leo Novemba 18. Katikati ni Spika wa Bunge, Anne Makinda na Mwenyekiti wa Umoja huo, Lediana Mg’ong’o wakishangilia uzinduzi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasha Mshumaa ikiwa ni ishala ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Umoja wa Wabunge wa Tanzania wa kupambana na Ukimwi (TAPAC), uliofanyika kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma leo Novemba 18. Katikati ni Spika wa Bunge, Anne Makinda na Mwenyekiti wa Umoja huo, Lediana Mg’ong’o wakishangilia uzinduzi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi Christoph Benn, wakati wa uzinduzi huo. Katikati ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge wa Tanzania wa kupambana na ukimwi, Lediana Mg’ong’o
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Umoja wa Wabunge wa Tanzania wa kupambana na Ukimwi (TAPAC), uliofanyika kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma leo Novemba 18.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR
No comments:
Post a Comment