Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, November 9, 2011

PSPF YAPEWA TUZO KWA KUTOA MIKOPO YA NYUMBA KWA WASTAAFU

Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudensia Kabaka akimkabidhi kaimu Mkurugenzi wa PSPF .Bw.Adam Mayingu tuzo ya kutambua juhudi za PSPF katika kutoa mkopo wa nyumba kwa wanachama wake wanaokaribia kustaafu wakati wa ufunguzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya hifadhi ya jamii iliyoanza katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam jana.
Kaimu Mkurugenzi wa PSPF .Bw.Adam Mayingu (kulia) akitoa maelezo ya shughuli waifanyayo kwa Waziri wa Kazi na Ajiram, Mh. Gaudensia Kabaka wakati wa ufunguzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya hifadhi ya jamii iliyoanza katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam jana.
Wafanyakazi wa PSPF wakifurahia tuzo waliyoipata baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudensia Kabaka wakati wa ufunguzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya hifadhi ya jamii iliyoanza katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam jana.tuzo hiyo ni kwa kutambua juhudi za mfuko huo katika kutoa mikopo ya nyumba kwa wanachama wake wanaokaribia kustaafu.
Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudensia Kabaka akijaza fomu ya uhakiki wa wastaafu wakati alipotembelea banda la PSPF katika maonesho ya Wiki ya hifadhi ya Jamii Mnazi Mmoja Dar es salaam jana Kabaka ni mmoja ywapo wa wastaafu wa PSPF kushoto ni Ofisa wa Fedha Mwandamizi Bw. Victor Luvena

No comments: