Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, November 9, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL MGENI RASMI ONESHO LA SANAA LA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Onesho maalum la Vyombo vya Ulinzi na Usalama (VUU) lililoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza Watanzania kwa kudumisha amani na Umoja katika kuelekea Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Onesho hilo lilifanyika jana jioni Novemba 8 katika Ukumbi wa Diamond jubilee Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi, wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana jioni Novemba 8, kufungua onyesho la maalum la Vyombo vya Ulinzi na Usalama (VUU) lililoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza Watanzania kwa kudumisha amani na Umoja katika kuelekea Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.
Wasanii wa Kwaya ya JKT, wakiimba jukwaani wakati wa Onesho maalum la Vyombo vya Ulinzi na Usalama (VUU) lililoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza Watanzania kwa kudumisha amani na Umoja katika kuelekea Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam jana jioni Novemba 8, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
Waimbaji wa Bendi ya Polisi wakiimba jukwaani wakati wa Onesho maalum la Vyombo vya Ulinzi na Usalama (VUU) lililoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza Watanzania kwa kudumisha amani na Umoja katika kuelekea Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam jana jioni Novemba 8. ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Wasanii wa ngoma ya asili wa kikundi cha Sanaa cha Polisi, wakionyesha umahiri wao jukwaani wakati wa Onesho maalum la Vyombo vya Ulinzi na Usalama (VUU) lililoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza Watanzania kwa kudumisha amani na Umoja katika kuelekea Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam jana jioni Novemba 8. ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.

Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Polisi, wakionyesha umahiri wao jukwaani wakati wa Onesho maalum la Vyombo vya Ulinzi na Usalama (VUU) lililoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza Watanzania kwa kudumisha amani na Umoja katika kuelekea Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam jana jioni Novemba 8. ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments: