Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, November 5, 2011

Mwenge wa uhuru utakimbizwa katika mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini kuanzia leo.

Na mwandishi wetu.
Mwenge wa uhuru utakimbizwa katika mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini kuanzia leo ambapo mwenge huo utaanzia mkoani Rukwa.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na kamati ya mbio za mwenge taifa, mwenge wa uhuru utawasili mkoani Rukwa novemba 5 hadi sita na kukabidhiwa mkoani Mbeya Novemba 7 hadi 8 kisha mwenge huo unaelekea mkoani Iringa.

Kwa mkoa wa Iringa mwenge wa uhuru utawasili novemba 9 hadi 10 na ziara yake itamalizika kwa mkoa wa Ruvuma ambapo mwenge huo utawasili Novemba 11 hadi 12.

Kauli mbiu ya mwenge wa uhuru mwaka huu ni TUMETHUBUTU, TUMEWEZA na TUNASONGA MBELE.

No comments: