Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, November 5, 2011

Makamu Wa Rais Dkt. Bilal Afunguo Mkutano Wa Mawaziri Wa Wizara Za Maendeleo Ya Wanawake Na Watoto Wa Nchi Za Maziwa Makuu- Arusha


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Wanawake na Watoto Zanzibar, Zainab Omar, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Arusha, kwa ajili ya kufungua rasmi Mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Maendeleo ya Wanawake na Watoto, wa Nchi za Maziwa makuu, ulioanza leo Novemba 4, katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mkuu wa Mkoa Arusha, Mulongo Magesa, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na Balozi Liberata Mulamula, wakati akiingia kwenye Ukumbi wa Mikutano wa AICC Mkoani Arusha kufungua mkutano wa wa Mawaziri wa Wizara za Maendeleo ya Wanawake na Watoto, wa Nchi za Maziwa makuu. Mkutano huo umefunguliwa leo Novemba 4.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika Ukumbi wa AICC, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo eliofunguliwa leo Nov 4, jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika Ukumbi wa AICC, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo eliofunguliwa leo Nov 4, jijini Arusha. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua Mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Maendeleo ya Wanawake na Watoto, wa Nchi za Maziwa makuu , uliofunguliwa leo Nov 4, katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments: