Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, November 16, 2011

Mradi wa MWEI wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania Watinga Mkoani Mwanza

Mratibu wa mradi wa MWEI wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Bw. Mgongo Emmanueley akitoa mafunzo ya awali kwa wanawake wa Usagara Mkoani Mwanza kuhusiana na mradi huo utakaowapa fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi katika biashara zao ndogondogo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya mradi wa MWEI unaoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania wakipata maelekezo ya kutumia huduma ya M-pesa kutoka kwa Mratibu wa mradi huo Bw. Mgongo Emmanueley wakati mafunzo hayo yenye kuwawezesha kujikwamua kiuchumi yakiendelea huko Usagara Mkoa wa Mwanza.
Kikundi cha wanawake kutoka Usagara Mkoani Mwanza wakipata maelekezo ya namna ya kutumia huduma ya M-pesa katika simu zao za mkononi kutoka kwa Mratibu wa mradi wa MWEI Bw. Mbuyu Ally unaoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania ukiwa na lengo la kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi na kuendeleza biashara zao ndogondogo.
Mratibu wa mradi wa MWEI unaoendeshwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Bw. Mgongo Emmanueley (wan ne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na kikundi cha wanawake wa Usagara Mkoa wa Mwanza mara baada ya kumalizika kwa mafunzo kuhusu mradi huo ambao pia utawawezesha kujikwamua kiuchumi kupitia biashara zao ndogondogo.


No comments: