Mgambo wa jiji wakifungua namba za gari iliyopaki maegesho yasiyoruhusiwa
HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya, imewafukuza kazi askari mgambo nane kwa kosa la kuhusika na unyanganyi wa bidhaa mbalimbali zinazotembezwa na wamachinga na baadhi ya wakina mama wajasiliamali.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, alisema hatua ya kuwafuta kazi askari hao ni kutekeleza sheria ndogo inayomtaka askari kutonyanganya mali au bidhaa ya mtu kwa maslahi yake binafsi.
Alisema, hivyo ofisi ilipokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara hao ambayo yalikuwa yakiwatuhumu askari hao kuchukua mali zao ambayo yalifanyiwa kazi na baadhi yao kukutwa na hatia hivyo halmashauri kuwafukuza kazi kwa mujibu wa sheria.
Alisema kazi ya askari wa Jiji si kunyanganya bidhaa za wafanyabiashara hao bali ni kuwazuia kutoendesha shughuli hizo kwenye maeneo ambayo yamepigwa marufuku.
“Hivyo baada ya ofisi kubaini kuwa askari hawa walihusika na ukiukwaji wa sheria kwa kuchukua bidhaa za wafanyabiashara hao kwa maslahi yao binafsi, tumehamua kuwafukuza kazi,”alisema
Alisema, kila mtu yupo katika utawala wa sheria na hakuna hata mmoja ambaye anaishi juu ya utawala huo hivyo kitendo cha kujichukulia madaraka ya kuwanyanga’nya bidhaa wafanyabiashara na kuondoka nazo ni ukiukwaji wa sheria hivyo wahusika wanahaki ya kupata adhabu hiyo.
Hata hivyo kiongozi huyo aliwaomba wakazi wa Jiji la Mbeya hususani wafanyabiashara wadogowadogo kutoa taarifa kwenye kitengo husika endapo askari wa Jiji yeyote yule atahusika na unyang’anyaji wa bidhaa na kuondoka nazo kwani kazi ya askari ni kuzuia watu wasifanye biashara kwenye maeneo ambayo yamepigwa marufuku na si kubeba bidahaa.
|
No comments:
Post a Comment