Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, October 28, 2011

WAZIRI NAGU AMEZITAKA TAASISI NA VYOMBO VYA DLA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI.


Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk. Mary Nagu
(katikati).
Na mwandishi wetu.
Waziri wa nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na uwezeshaji Dkt.Mary Nagu (Mb) amezitaka taasisi na vyombo vya dola kuweka mazingira wezeshi ili kuboresha mazingira ya kufanya biashara kwa wawekezaji katika Tanzania ili kusiwepo na vikwazo na ucheleweshwaji wa huduma muhimu.

Dkt. Nagu aliyasema hayo jana wakati wa ufunguzi wa kituo cha uwekezaji kwa kanda ya nyanda za juu kusini kilicho ofisi za Bank ya NBC Jijini hapa.

Alisema kuwa ili wawekezaji wa kanda ya Mbeya waweze kufanya kazi vizuri hakuna budi vikwazo vyote kuondolewa na upatikanaji wa huduma muhimu kwa wawekezaji urahisishwe.


Hata hivyo waziri Nagu alihimiza mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kuendelea kutenga, kupima na kusajili maeneo ya uwekezaji ipasavyo kabla ya kuyagawa pale inapowezekana ili kuondoa usumbufu ambao unaweza kujitokeza.

Alisema ikumbukwe kuwa uwekezaji ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa nchi kwani utaongeza pato la Taifa, mitaji na teknolojia na ajira kwa watanzania wengi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kituo cha Uwekezaji cha Tanzania Balozi Elly Mtango alisema kituo hicho kinategemea kufanya kazi na mamlaka nyingine za mikoa na serikali za mitaa na vijiji katika kufanikisha upatikanaji wa maeneo kwa ajili ya shughuli za uwekezaji na uendelezaji wa miuondo mbinu.

Aidha alitoa wito kwa wafanyabishara na wawekezaji wote katika kanda ya mbeya kutumia kituo hicho katika kujipatia huduma mbali mbali ili wajiendeleze kibiashara na kiuwekezaji.

1 comment:

Anonymous said...

Mahodari kusema si kutekeleza...yeye alipokuwa waziri wa viwanda alikuwa hayajui hayo.... wahindi tu ndio aliwakumbatia...tusidanganyane na siasa zao...kwamnza tumewachoka kupita kiasi.