Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, October 22, 2011

WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI + MBEYA




Na mwandishi wetu
Watu wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti mkoani Mbeya likiwemo tukio la mlinzi mmoja kuuwawa na watu wanadhaniwa kuwa ni majambazi eneo la Iwambi jijini Mbeya.

Akiongea na waandishi wa habari kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Anecletusi Malindisa amesema Godfrey Anjero mwenye umri wa miaka 48 ambaye anafanya kazi ya ulinzi wa kujitegemea amekutwa ameuawa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi ambao walivunja na kuiba maduka matatu yaliyopo eneo la Maduka Iwambi jijini Mbeya.

Amesema mwili wa Anjero umekutwa ukiwa umefungwa mikono na kuzibwa mdomo kwa kutumia kipande cha nguo huku ukiwa na majeraha ambayo yametokana na kukatwa katwa kwa kutumia kitu chenye ncha kali.

Aidha amesema Ally Mwapala mwenye umri wa miaka 22 mkazi wa kijiji cha Mlale wilayani Ileje mkoani Mbeya amefariki dunia baada ya gari lenye namba za usajili T.463 BRJ kuacha njia na kupinduka eneo la Mapogoro barabara ya Mpemba na kusababisha majeruhi kwa watu watatu.

Ameongeza kuwa Jeshi la polisi linamtafuta Dereva wa gari hilo Oswadi Bugapi ambaye alikimbia mara baada ya ajali kutokea na kwamba uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha ajali hiyo.

No comments: