Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, October 18, 2011

WADAU MSAADA KWA KIJANA ALIYEA ATHIRIKA UTI WA MGONGO BAADA YA KUANGUKA AKIWA MACHIMBONI MERELANI

Na mwandishi wetu.
Kijana Ismail Omary Shabani mwenye umri wa miaka 23 anaomba msaada wa shilingi elfu 50 ili aweze kununua dawa zitakazomwezesha kumpa nguvu ya kutembea baada ya kupata ajali machimboni ya kuanguka na kuathirika kwenye uti wa mgongo.

Akizungumza na Chimbuko letu na kushuhudia kijana Ismail akihitaji msaada wa kushiliwa kwa umakini ili aweze kutembea, amesema tatizo hilo alilipata katika mgodi wa Merelani mwezi August mwaka jana ambapo huduma ya matibabu imeipata katika hospitali za KCMC na Muhimbili.

Mpaka sasa anahitaji dawa za CC 10 za Sindano na Vidonge 60 vinavyoitwa Baikrofeneki ambapo jumla ya gharama za dawa na sindano hizo ni shilingi elfu 50.

Chimbuko letu inaiomba jamii kwa pamoja kushirikiana kumsaidia kijana huyo ili aweze kurejesha upya hali yake kwa kutoa mchango wako wa kiasi chochote kupitia simu namba 0766 332339.

No comments: