Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, October 18, 2011

RAIA MMOJA WA CHINA AMEFARIKI DUNIA NA WATATU KUJERUHIWA BAADA YA GARI KUACHA NJIA NA KUPINDUKA ENEO LA MSWISWI - MBARALI - MBEYA

:

Na mwandishi wetu
Mkazi mmoja Kongolo Kyiyu Owoju mwenye umri wa miaka 45 Raia wa China amefariki dunia ka ajali ya gari juzi, maeneo ya Mswizi wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya na watu watatu kujeruhiwa baada ya gari lenye namba za usajili T 625 ANH aina ya Honda CRV kuacha njia na kupinduka.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Anacletus Malindisa amesema dereva wa gari hilo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu pamoja na majeruhi watatu ambao ni Housh Youni mwenye umri wa miaka 15, Peong Fongwi mwenye umri wa miaka 58,na Hong Weiy mwenye umri wa miaka 56 wote ni raia wa CHINA.
Aidha Malindisa amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi majeruhi wamelazwa katika hospitali ya Chimala na gari lipo kituoni Chimala.

Aidha amesema Jeshi aPolisi limemshikilia Veronica George mkazi wa Isansa Wilayani Mbozi kwa kosa la kumtumbukiza mtoto wake wa kike mwenye umri wa siku tatu.

Veronica amemtumbikiza mtoto huyo baada ya mumewe aitwaye Majaliwa Mwampashi kukataa kwamba mtoto huyo si wake.

No comments: