Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, October 15, 2011

Sherehe za kuwasha mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa kijijini butiama Jana

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Mwenge wa uhuru kiongozi wa mbia za mwenge huo mwaka 2011 2012 Mtumwa Rashid Halfan kutoka mkoa wa kaskazini Unguja, kwa ajili ya kuanza mbio za kukimbiza katika mikoa yote ua Tanzania baada ya kuuwasha rasmi leo katika kijiji cha Butiama Mkoani Mara.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la mauwa kwenye Kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalim Julius Nyerere baada ya misa maalum ya kumkumbuka muasisi huyo Taifa la Tanzania iliyofanyika leo kijijini kwake Mwitongo Butiama.
Mwandishi wa Habari na mpiga picha mwandamizi wa Idara ya Habari Maelezo Bi. Anna Itenda, kwa niaba ya waandishi wa habari wa Tanzania, akiweka shada la mauwa katika kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwalim Julius Nyerere wakati wa misa maalum ya kumkumbuka muasisi wa Taifa la Tanzania iliyofanyika jana kijijini Mwintongo Butiama.
Picha zote na Amour Nassor wa VPO

No comments: