Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, October 15, 2011

MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA MBEYA MHESHIWIWA KAPUNGA AMWAGIZA MKURUGENZI WA JIJI KUANDAA SEMINA KWA MADIWANI.


*****
Na mwandishi wetu
Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, kuandaa semina haraka kwa Madiwani wa Halmashauri hiyo ili kuwaelimisha juu ya kanuni za uendeshaji wa vikao vya Halmashauri.

Kapunga ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na tamko la CHADEMA, ambalo walilitoa wakimtaka ajiuzulu wadhifa wake.

Aidha agizo hilo la Meya limekuja ikiwa ni siku mbili baada ya madiwani CHADEMA, kususia kikao cha Baraza la Madiwani, kitendo ambacho KAPUNGA anaamini kimechangiwa na madiwani hao kutokuzijua kanuni na sheria za uendashaji wa vikao vya Baraza la Halmashauri.

No comments: