Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, October 21, 2011

MWALIMU AKUTWA AMEUWAWA NA MWILIWAKE KUACHWA MTUPU NA KUHARIBIKA VIBAYA MBEYA

Na mwandishi wetu
Mwalimu wa shule ya msingi Wimba iliyopo tarafa ya Igale B. kata ya Utengule Usongwe Bi.Maria Harudo Sanga mwenye umri wa miaka 46 amekutwa ameuawa na mwili wake kuachwa ukiwa mtupu na kuharibika vibaya.

Akiongea na mwenyekiti wa Kijiji cha wimba Dickson Mlawa amesema October 14 mwaka huu mwalimu huyo aliaga kwenda Iringa baada ya kuibiwa vitu vya thamani kwenye nyumba yake na kwamba hakuonekana kwa zaidi ya siku 4 hadi hapo mwili wake ulipokutwa ukiwa umeharibika

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Wimba Nikubuka Mbwile amesema taarifa za kifo cha mwalimu huyo zilitolewa na wanafunzi baada ya kukuta nguo za mwali huyo kichakani

Nao wanafunzi wa shule hiyo Ayubu Japheti na Erenesi Wile wamesema nguo za mwalimu wao waliziona wakati wakiwa wanaelekea kwenda shule.

Naye kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Anecletusi Malindisa amekiri kutokea kwa mauaji hayo na kusema kuwa uchunguzi zaidi bado unaendelea.

Imeelezwa kuwa wakati wa uhai wake mwalimu huyo alikuwa na kesi 4 katika mahakama ya hakimu mkazi Mbeya akiwadai watu watano fedha ambapo katika kesi hizo mwalimu huyo alishinda na kupewa haki yake.

No comments: