Na mwandishi wetu. Zaidi ya shilingi milioni moja na laki tatu zimetumiwa na halmashauri ya wilaya ya Ileje mkoani Mbeya kwa kuhamasisha wakulima kujiunga kwenye vikundi vya wakulima pamoja na kuhamasisha ujenzi na matumizi ya maghara bora ya kuhifadhia mazao. Hayo yameelezwa na mkuu wa wilaya ya Ileje Bi Ester Wakari wakati wa mahojiano ofisini kwake kuhusu namna ambavyo wilaya hiyo imewasaidia wakulima elimu ya uhifadhi wa mazao gharani. Bi.Wakari amesema kwa kutumia fedha hizo wamefanikiwa kutoa elimu kwa SACCOS kumi na kuhamasisha wananchi kujiunga kwenye vikundi ili waweze kuwa na mipango madhubuti ya kuhifadhi na kuuza mazao yao kupitia mfumo wa stakabathi gharani. Wakati huohuo amesema kuwa wakulima wamehamasishwa kupima mashamba yao ili waweze kupata hati miliki za kimila zitakazo wasaidia kuwarahisishia kupata mikopo kutoka kwa taasisi mbalimbali za kifedha ambapo mpaka sasa wakulima 280 wamekwisha pimiwa maeneo yao na kupewa hati miliki za kimila.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment