Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, September 15, 2011

UBOVU WA MIUNDOMBINU, BEI KUBWA KWA PEMBEJEO ZA KILIMO YASABABISHA WAKULIWA WA ZAO LA VIAZI KUTONUFAIKA NA ZAO HILO.

Na mwandishi wetu. Wakulima wa viazi kijiji cha Lusanje kata ya Mpombo Mwakaleli wilayani Rungwe mkoani Mbeya wamesema kupanda bei kwa pembejeo za kilimo na ubovu wa miundombinu imekuwa ikichangia wao kutonufaika na kilimo hicho. Mmoja wa wakulima wa viazi hivyo Gilibert Mwasanteba amesema bei ya Mbolea ya kukuzia na kupandia na dawa za kuua wadudu zimepanda hali inayowafanya kutumia gharama kubwa kwa kilimo kuliko kipato kinachopatikana Wakati huohuo ametoa ombi kwa Serikali kuongeza vocha za ruzuku kutokana na mfumo unaotumiwa sasa wa vocha moja ama mbili kutolewa kwa mkulima mmoja kutoendana na ukubwa wa shamba linalolimwa.

No comments: