Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, September 29, 2011

Wanafunzi Nchini watakiwa kuzingatia masomo zaidi kulipo Siasa

Na Esther Macha, Mbeya

WANAFUNZI nchini wametakiwa kuachana  na tabia ya kuzama kwenye siasa na badala yake kuzingatia  kujiendeleza na elimu ya juu kwani walioko kwenye siasa  wana elimu zao.

Imeelezwa kuwa idadi kubwa ya wanafunzi wamekuwa wakikimbilia kwenye siasa kuliko masomo ambayo ndiyo yamewapeleka  mashuleni na hivyo siku ya siku kubaki wakimbulia kufeli mitihani yao ya mwisho.

Akizungumza wakati wa mahafali ya pili ya kidato cha nne ya shule ya sekondari ya Itebwa Mwenyekiti wa chama cha  kuweka na kukopa cha Walimu wa Sekondari Wilaya ya Mbeya Vijijini Bw.Frank Phili alisema kuwa huo si wakati wa kujiingiza kwenye siasa kwa wanafunzi na kwamba wanafunzi wasikubali kutumika kwani watavuruga
masomo yao hivyo kujikuta kufanya vibaya katika masomo.

Alisema siasa ziwe na kiasi kwa wanafunzi kwani hapo hata kidato cha nne bado mwanafunzi yupo kwenye siasa huyo muda wa kusoma anaupata wapi alihoji  Mwenyekiti huyo .

Hata hivyo alisema tatizo hilo limeingia kwa vijana  zaidi walioko mashuleni  na limekuwa kama ugonjwa fulani sugu kwani wanachotakiwa ni kusoma kwanza siasa badaye, suala la siasa limekuwa ni tatizo kwa wanafunzi waliopo vyuoni  na mashuleni  am,balo limekuwa na sawa na ugonjwa usiopona .

"Ndugu zangu siasa iwe kiasi  msiweke akilini  sana kwani hata wanasiasa waliopo wamesoma sana sasa nyie ndugu zangu mkijiweka sana kwenye siasa mtakuja kulia kwa hapo baadaye umri wenu ni mdogo sana"alisema.

Akisoma risala kwa niaba ya Wanafunzi  wenzake wanaomaliza kidato cha nne Bw. Lusekelo William alisema kuwa wanamaliza kidao cha nne wakti shule  hiyo iiwa haina vifaa vya maabala na hicvyo kusababisha  wanafunzi kuchukia masomo ya sayansi.

“Shule kuwa na baabala iliyokamilika inasaidia kuongeza ujuzi na
 maalifa kwa Wanafunzi  hivyo  kuweza kufanikiwa kuendelea kimasomo na kufanikiwa kufanya vizuri katika ngazi ya chuo”alisema

Awali akisoma taarifa ya shule Mkuu wa shule hiyo Bw. Mpege Mwankotwa
  alisema kuwa jumla ya wanafunzi 89 wamehitimu elimu ya kidato cha nne katika shule hiyo ambpo alisema kuwa shule hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbali mbali.

Bw.Mwankotwa alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na Maabaala kukosa
  vifaa,Wazazi na  Walezi kutolipa ada kwa wakati na kusababisha kuwepo kwa maendeleo hafifu kwa wanafunzi.

Kwa upande  Mwenyekiti wa chama cha  kuweka na kukopa cha Walimu wa
  Sekondari Wilaya ya Mbeya Vijijini Bw.Frank Phili aliwataka wanafunzi wanaohhitimu kuzingatia masomo waliyofuindishwa na darasani ili kuweza kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho.


No comments: