SERIKALI YAOMBWA KUANZISHA VYUO VYA UDEREVA PIKIPIKI ILI WAWEZE KUZIJUA SHERIA ZA BARABARANI
Na mwandishi wetu.
Wadau wa usafirishaji mkoa wa Mbeya wameiomba Serikali kuanzisha vyuo vya udereva wa pikipiki ili kuwawezesha madereva wa pikipiki na bajaji kuzijua sheria za barabarani.
Ombi hilo limetolewa na wakazi wa mtaa wa Mwanjelwa jijini Mbeya wakati wa mahojiano na mwandishi wetu juu ya namna wanavyoweza kushirikiana na Serikali kupunguza matukio ya ajali za pikipiki.
Wamesema uelewa mdogo wa madereva wa pikipiki kuhusu sheria za barabarani ndio chanzo kikubwa cha ajali za pikipiki na ufumbuzi wa tatizo hilo ni madereva kutokupewa leseni mpaka watakapo kuwa wamepitia vyuo vya udereva wa pikipiki.
Kwa upande wao madereva wa pikipiki Bwana Joseph Mbwilo na Bwana Issa Nziku wamesema ili kukabiliana na tatizo la ajali zitokanazo na uzembe wa baadhi ya madereva wa pikipiki, wamiliki wa pikipiki wanatakiwa kuajiri madereva walio na elimu ya usalama barabarani.
No comments:
Post a Comment