Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, September 23, 2011

MJI MDOGO WA TUNDUMA HALI SI SHWARI KWA WAFANYABIASHARA


.

Na mwandishi wetu.
Kufuatia kuchelewesha kwa matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Zambia, milipuko ya mabomu imekuwa ikilindima siku ya jana kuanzia majira ya saa 4 asubuhi wilayani Nakonde nchini humo hali iliyopelekea kuwa si shwari katika mji mdogo wa Tunduma kutokana na ukaribu uliopo wa kibiashara.

Kuanzi majira ya 7 mchana maduka yalikuwa yemefungwa huko Tunduma na wengine kuhabisha bidhaa zao kutoka nje ya mji huo wakihofia kuibiwa au kuvuinjwa kwa maduka yao kutokana na ukaribu wa eneo la tukio.

Mtandao huu ulipata kushuhudia milipuko hiyo mfulululizo mpaka majira ya saa 1 usiku ambapo iliwafanya baadhi wa Wanazambia waliokamilisha kupata kibali cha kuvuka mpaka,  kushindwa kushindwa kuvuka mkapa kuelekea nchini mwao.

Hata hivyo mrundikano wa Magari ulikuwepo mpakani hapo na watu kuhofu  kuvuka mpaka kutokana na mabasi mawili ya Kampuni ya Falcon na Taqwa kurudishwa kutokana na machafuko, kwa taarifa zilizopo kuwa toka Septembe 17, mwaka huu magari ya abiria nchini zambia yalisitisha kutoa huduma ya usafirishaji kutokana na hali hiyo ya sitofahamu ya uchaguzi uliofanyka siku ya Jumanne wiki hii.

Shuhuda kutoka Tunduma aitwaye Bwana Alex Kajumulo ambaye hufanya shughuli zake mji wa Kapirimposhi ameshindwa kufanyabiashara nchini humo na kuambua kurejea nchini Tanzania kutokana na hali ya machafuko nchini Zambia.

Mvutano mkali upo kati ya Chama cha siasa cha Upinzani ya UPF  kinachongozwa na Bwana Michael Sattah na Chama tawala cha MMD kinachoongozwa na Bwana Rupia Banda. ambapo wapinzani wanadai wameshinda uchaguzi huo na kwamba Serikali inataka kuchakachua matokeo hayo na kusababisha machafuko nchi nzima.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Tunduma Mheshimiwa Frank Mwakajoka amesema hali hii imepelekea wajasiriamali na wafanyabiashara katika kata yake kushindwa kufanya biashara tangu jana, ambapo inawatia hofu kiuchumi kwani Wilaya ya Nakonde na Tunduma zinategemeana kibiashara.

Kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa wa Mbeya ilikutana jana mchana, ili kupanga mikakati ya kuimarisha Ulinzi na usalama mpaka.

No comments: