Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, September 28, 2011

MATUKIO YA UPIGAJI NONDO MKOANI MBEYA YAIBUKA KWA KASI MPYA

Bwana Elia Daudi Mwalonde mkazi wa Uyole akiwa hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya wodi namba 1 baada ya kupigwa nondo.
=====
Na mwandishi wetu.
Matukio ya upigaji Nondo jijini Mbeya yameibuka kwa kasi mpya ambapo watu kadhaa wamekwisha poteza maisha na wengine wamesababishia ulemavu wa kudumu.

Baadhi ya maeneo ambayo wananchi wamekuwa wakipigwa Nondo ndani ya jiji hili ni Ilemi, Isanga, mabatini, Air Port, Uyole, Mwanjelwa na Soweto.

Kutokana na kuibuka kwa vitendo hivyo Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi ametangaza vita dhidi ya wanaojihusisha na vitendo hivyo na kusema kuwa doria imeanza rasmi ili kuwabaini wahusika.

Wakati huohuo amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za siri ambazo zitafanikisha kukamatwa kwa watu hao wanaojihusisha na vitendo vya upigaji Nondo.

2 comments:

Anonymous said...

inasikitisha sana kwa kweli

Anonymous said...

polisi mbeya mnafanya kazi gani. au mnasubiri mpaka kamanda wenu nyombi apigwe nondo ndo muamke.