Na mwandishi wetu.
Zaidi ya waathirika 35 wa janga la moto katika soko la Mwanjelwa Sido wamekosa maeneo ya kujenga vibanda vyao upya baada ya kutolewa kwa tangazo linalowataka wafanyabiashara 969 waliounguliwa na soko la Mwanjelwa kuendelea na ujenzi huku wale wengine wakisubiri kupangiwa maeneo mengine upya.
Agizo hilo lilitolewa na mkuu wa mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro alipotembelea sokoni hapo wiki mbili zilizopita ambapo amesema kuwa zoezi la uokoaji wa mali za watu lilichukuwa muda kumalizika kutokana na ujenzi holela uliokuwepo awali sokoni hapo.
Katibu wa soko la sido Bwana Alanus Ngogwe amesema kuwa wafanyabiashara waliokosa maeneo ya kujenga vibanda vyao upya wanaendelea kulishughulikiwa tatizo hilo na kuongeza kuwa endapo yatakosekana maeneo wafanyabiashara hao watahamishiwa katika masoko mengine.
Wakati huohuo amesema kuwa soko hilo limeanza kutoa huduma ambapo biashara zinazoendelea kutolewa hivi sasa ni pamoja biashara za mitumba, viatu, viazi, machungwa, ukindu na nafaka.
No comments:
Post a Comment