Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika Viwanja vya Maisala mjini Unguja, wakati alipotembelea katika eneo hilo lililokuwa likitumika kupokelea miili ya watu waliofariki katika ajali ya meli ya Spice jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na kumpa pole mmoja kati ya wakazi wa Unguja waliopotelewa na ndugu katika ajali ya meli ya Spice iliyotokea eneo la Nungwi, wakati makamu alipotembelea majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea na kukagua maeneo yaliyokuwa yakitumika kupokelea na kuhifadhi miili ya watu waliokufa katika ajali ya meli ya Spice, pamoja na majeruhi waliokuwa wakipitishwa katika eneo hilo la Ufukwe wa Bahari ya Hindi Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja le.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, wakati walipokutana katika viwanja vya Maisala, walipofika kutembelea mabanda ya kupokelea miili ya watu waliofariki katika ajali ya meli ya Spice jana
Makamu wa Rais, Dkt Bilal, akiondoka katika eneo hilo baada ya kuzungumza na wananchi wa Nungwi na kuwapa pole na hongera kwa huduma walizotoa katika waathirika wa ajali hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wakazi viongozi na wakazi wa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati alipofika katika eneo hilo kwa ajili ya kuwafariji wakazi hao waliopatwa na matatizo pamoja na kukagua shughuli za uokoaji, leo.
Hata hivyo baadhi ya wananchi wametoa maoni yao kuhusiana na jitihada za Serikali na watu binafsi katika kutoa huduma za uokoaji, ambapo walisema kuwa katika ajali zote zilizokwishatokea haikuahi kutokea waathirika kupata huduma ya haraka kama hii ambapo hadi vyombo binafsi vya usafiri vliliweza kuhamasika na kuelekea eneo la tukio kutoa msaada.
Baada ya Rais kutembele eneo la tukio leo hii, ameagiza wataalam wa DNA nao kufika eneo hilo kwa ajili ya kuweza kutambua wale watakaokuwa wamewakosa ndugu zao kupitia vipimo maalum Sayansi ya Vianasaba, ambapo tayari madaktari bingwa wamekwishawasili Unguja kwa kuanza zoezi hilo.
Wakati huo huo, wataalam wa uogeleaji na kupiga mbizi 'Wazamiaji' kutoka Afrika ya Kusini wanatarajia kuwasili kesho eneo la tukio kwa ajili ya kuungana na wataalam wa nchini katika kutafuta miili iliyonasa katika meli hiyo.
No comments:
Post a Comment