Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, September 10, 2011

CCM NA CHADEMA ZAKAMILISHA URUDISHAJI WA FOMU ZA KUWANIA NAFASI YA UDIWANI JIJINI MBEYA


Chama cha mapinduzi na Chama cha Demokrasia na maendeleo vimekamilisha zoezi la uchukuaji na urudishwaji wa fomu za kuwania nafasi ya udiwani kwa kata ya Majengo na Nzovwe.

Akizungumza na mwandishi wetu katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mbeya mjini.BAHATI MAKALANZI amesema katika uchaguzi huo chama chake kitawakilishwa na SAMUEL MWAMBONA kwa kata ya Majengo na ISAAC SINTUFYA kwa Kata ya Nzovwe ambao wote wamerudisha fomu kwenye ofisi za kata.

Naye Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya Mjini CHRISTOPHER MWAMUSIKU amesema chama chake kitawakilishwa na JOSEPH MWASAMPETA kwa kata ya Majengo na Mchungaji DAVID MWASHILINDI kwa Kata ya Nzovwe ambao wote wamekwisha rudisha fomu kwenye ofisi za kata.

Kampeni kwa ajili ya kuwania nafasi ya Udiwani kwa kata hizo mbili zilizoachwa wazi zitaanza kesho na uchaguzi utafanyika octoba pili mwaka huu.

No comments: