NA FRANCIS GODWIN
MZIMU wa ajali waendelea kuandama mkoa wa Mbeya baada ya juzi watu watatu kupoteza maisha kwa kugongwa la Lori eneo la Mbalizi mkoani Mbeya ajali nyingine imetokea usiku huu katika Mlima wa Msangamweli mpakani mwa Mbeya vijijini na wilaya ya Chunya.
Mwandishi wa mtandao huu kutoka Mbeya Moses Ng'wat anaripoti kuwa ajali hiyo imehusisha lori ambalo lilikuwa limebeba wafanyabiashara kutoka mnadani wilaya ya Chunya na baada ya kufika katika eneo hilo la Mlima Msamweli lilishindwa kupanda mlima na kupinduka ,inasemekana watu zaidi ya 10 wamepoteza maisha huku wengi wao wakijeruhiwa vibaya .
No comments:
Post a Comment