Wakazi wa eneo la Mwakibete mtaa wa viwandani wameuomba uongozi wa chuo kikuu cha Teofilo Kisanji kwa kushirikiana na halmashauri ya jiji la Mbeya kujenga dampo ili kuwaepusha wanafunzi wa chuo hicho pamoja na wakazi dhidi ya magonjwa ya milipuko.
Wakiongea na Mwandishi wetu Greyson wakazi wa mtaa huo wamesema kuwa dampo hilo limekaa kwa zaidi ya miaka mitano ambapo uzoaji wa taka umekuwa ukisuasua kutokana na ufuatiliaji hafifu wa uongozi wa chuo hicho.
Mmoja wa wakazi wa mtaa huo Bi.Edina Mbwilo amesema kuwa dampo hilo ni hatari kwa afya zao kutokana na kutoa harufu mbaya, ikiwa ni pamoja na kuhatarisha magonjwa ya milipuko kwa watoto ambao wamekuwa wakicheza kwenye dampo hilo.Naye Afisa utawala wa chuo Bwana Sichone amesema kuwa kuna hatua mbalimbali walizozichukua ili kuondoa dampo hilo kama vile kuzungushia wigo lakini hawakufanikiwa kutokana na watu kuendelea kutupa taka katika eneo hilo na kuongeza kuwa uongozi wa chuo uko mbioni kuweka tangazo litakalo toa tahadhari juu ya matumizi ya dampo hilo.
No comments:
Post a Comment