Mkuu wa mkoa wa Mbeya John Mwakipesile amezitaka halmashauri zote mkoani Mbeya kutenga asilimia 15 za pato lake ili kuwasaidia wakulima kupata pembejeo za kilimo.
Rai hiyo ameitoa wakati wa maadhimisho ya kumi ya Tanzania coffee research institute (TACRI) yaliyofanyika wilayani Mbozi ambapo kitaifa yatafanyika mkoani Kilimanjaro Septemba 9 mwaka huu.
Mwakipesile amesema kutokana na zao la kahawa kuingiza pato kubwa Serikalini, haina budi halmashauri kuwasaidia wakulima wa zao hilo ili waweze kuzalisha kwa wingi.
Ameongeza kuwa kupitia zao la kahawa nchi imekuwa ikijipatia fedha za kigeni zaidi ya shilingi milioni 200 kwa mwaka pamoja na kupunguza umasikini kwa wakazi zaidi ya laki moja na nusu kutoka mikoa ya Mbeya na Rukwa.
No comments:
Post a Comment