Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bwana JOHN MWAKIPESILE amewataka wakurugenzi wa halmashauri na wakuu wa idara kusimamia sheria na miongozo ya serikali katika ukusanyaji mapato na matumizi ya fedha ambazo zinatolewa na serikali kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani wilaya Mbarali kilichokuwa kikijadili taarifa ya ukaguzi na udhibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG) alisema ni vyema wakuu hao wakisimamia sheria hizo ili fedha za miradi ya maendelo ambazo zinatolewa na serikali ziweze kutumika kwa malengo yanayokusudiwa.
Pia ametoa angalizo kwamba viongozi wanapaswa kuungana pamoja ili kudhibiti matumizi mabaya ya fedha hizo na kutekeleza jukumu la kuwainua wananchi kwa vitendo.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri wilaya hiyo Bwana GEORGE KAGOMBA amesema halmashauri imekuwa ikizingatia kanuni na miongozo ya serikali katika ukusanyaji mapato.
No comments:
Post a Comment