Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, August 4, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATEMBELEA MABANDA MAADHIMISHO YA PILI YA NANE NANE MJINI DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi funguo ya Trekta la kilimo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Teresia Huvisa, kwa ajili ya matumizi ya kilimo, wakati wa hafla ya maadhimisho ya mwaka wa pili wa utekelezaji wa Kaulimbiu ya Kilimo Kwanza leo Agosti 03, 2011 ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya Nane Nane zinazoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Julius Niingu, wakati alipotembelea katika Banda la Ofisi ya Makamu wa rais. Wa pili kulia ni Mama Asha Bilal, wa pili (kushoto) ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Deo Magazeni.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakisikiliza maelezo kuhusu matumizi ya Trekta dogo la mkono (Power Tila) linalotumika kwa Kilimo, wakati wa hafla ya maadhimisho ya mwaka wa pili wa utekelezaji wa Kaulimbiu ya Kilimo Kwanza leo Agosti 03, 2011 ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya Nane Nane zinazoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya Tela la Trekta linalotengenezwa nchini, wakatiti wa wakati wa hafla ya maadhimisho ya mwaka wa pili wa utekelezaji wa Kaulimbiu ya Kilimo Kwanza leo Agosti 03, 2011 ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya Nane Nane zinazoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Kilimo na Mbogamboga na Matuda, Hery Ndumukwa, kuhusu zao la Nyanya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijaribu kubeba shina la Muhogo, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika viwanja vya Nzuguni Nane Nane mjini Dodoma leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia na kusikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa kutoka Kituo cha kudhibiti Panya Mkoa wa Morogoro, Eugen Ngolohela, kuhusu Panya aina ya Ndezi na wengineo, wakati alipotembelea katika mabanda ya maonyesho ya Maadhimisho ya Nane Nane leo katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma. 
Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments: