Kilimo Kwanza jamanii, Mwanamke na Maendeleo afanye kazi asonge mbele
Zao la Nyanya
Wakulima wa mazao ya mahindi, nyanya, kabeji, ngano na njegele katika eneo la Uyole jijini Mbeya wamesema kupanda kwa bei za pembejeo za kilimo kumechangia kupanda kwa gharama za maisha.
Wakiongea nasi katika soko kuu la Uyole baadhi ya wakulima hao wamesema licha ya kuzalisha mazao mengi bado kipato chao ni kidogo kutokana na pembejeo za kilimo kama vile mbegu, mbolea na madawa kuwa na gharama kubwa
Wamesema kutokana na gharama hizo wamekuwa wakishindwa kufikia malengo yao baada ya kilimo kutokana na kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kupata pembejeo.
No comments:
Post a Comment