Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, August 7, 2011

Hapa na Pale Mkoani Mbeya

WANANCHI NA WENYEVITI WAKANA KUHAMA HIFADHI YA TAIFA RUAHA
Aina ya ndege waliopo hifadhi ya Ruaha
Wananchi na Wenyeviti wa serikali za vijiji 14 katika wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wamepinga agizo la serikali kuwataka wahamie ndani ya hifadhi ya taifa Ruaha kwa lengo la kuhifadhi bonde la Usangu ambalo ni chanzo kikuu cha maji ya mto Ruaha.

Wananchi hao wamesema hawapo tayari kwa kuwa historia inaonesha kwamba wezao wa vijiji jirani walihamishwa miaka ya nyuma walipunjwa kwa kulipwa fidia ya shilingi elfu 4 ambazo hazilingani na thamani ya mali walizokuwa nazo.

Mmoja wa wakazi hao Bwana Mponeja amesema hawapo tayari kufa masikini kama wezao waliohamishwa miaka ya nyuma kutokana na hali ngumu ya kimaisha.

UJENZI WA JOSHO KATA YA LUHANGA WAKAMILIKA.
Zaidi ya shilingi milioni 24 zilizochangwa na wafungaji wa kijiji cha Luhanga wilayani mbarali mkoani Mbeya zimetumika kukamilisha ujenzi wa josho la kuongeshea mifungo.
Katika fedha hizo shilingi milioni 20 ni mchango wa umoja wa wafungaji na shilingi milioni 4 zimetolewa na halmashauri ya wilaya ya Mbarali.

Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa josho hilo Saidi Nyang'ondo amesema josho hilo lina kina cha urefu wa futi 9.

Naye katibu wa kamati ya ujenzi huo Charles Juma amesema kukamilika kwa ujenzi huo kutasaidia kuwakinga ng’ombe dhidi ya magonjwa mbalimbali ukiwemo ugonjwa wa Ndigana.

No comments: